Waziri wa Nishati Mhe.DKt.Medard Kalemani (Mb) amefanya Ziara mkoa wa Mwanza na kuzindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu katika vijiji vya wilaya ya Magu.
Akiwa wilayani Magu Mhe.Dkt. Kalemani amewasha umeme na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuunganishiwa nishati hiyo ya umeme kwa gharama nafuu ili kuchochea maendelea ya kiuchumi katika maeneo yao.
Waziri Dkt.Kalemani katika ziara yake ametembelea Jumla ya vijiji vitatu ikiwemo kijiji cha Isangijo,Bulalo pamoja na Mahaha.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akimkaribisha Mhe Dkt.Kalemani amesisitiza kuwa Shule ya sekondari Mahaha iliyokuwa imekamilika tokea mwaka 2017 ifikapo tarehe 1 mwezi wa nane iwe imefunguliwa kwa kuwa ni moja ya changamoto ambazo wananchi wamepaza sauti.
Aidha Waziri Dkt Kalemani ameahidi kuchukua changamoto hiyo ya elimu na maji na kuzipeleka kwa mawaziri mwenye dhamana ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo Mhe.Dkt.Kalemani amemuacha Mkandarasi katika Kijiji cha Mahaha ili aanze kuwasha umeme kitongoji cha madukani A na B baada ya hapo wataendelea vitongoji vingine bila kuacha nyumba yoyote iliyolipia elfu 27.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.