Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameziagiza taasisizinazojihusisha na masuala ya bima nchini kujikita zaidi maeneo yavijijini kutoa elimu badala ya kupigana vikumbo mjini wakigombaniawateja ambako wananchi wana uelewa na kipato cha kujitibu mudawowote.
Agizo hilo alilitoa jana wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bimayanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza katika viwanja vya jengo labiashara la kimataifa la Rocky City Mall ambapo alisema anashangazwa kuonataasisi za bina zikiendelea kupambana katikati ya mjini wakativijijini kuna uhitaji mkubwa.
"Kama tunavyojua sekta ya bima ni sekta nyeti, muhimu na ina mchangokwenye uchumi wa taifa, ninatambua kuwa taasisihizi zinafanya kazi kubwa kwa ni bima yenyeweina faida nyingi sana kwa sababu ili biashara na shughuli zote za uzalishajimali ziwe na uhakika wa usalama kimsingi zinatakiwa kukatiwa bima.
"Hivyo niwaombe endeleeni kutoa elimu kwa watu wamakundi yote kwani kuna baadhi yao bado wanamini na wanaichukuliabima kama gharama na kusahau kuwa unapokuwa na bimaunakuwa kwenye mikono salama.
"Labda tu niwakumbushe wananchi wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla bimani gharama ila unapokuwa nayo unakuwa na amani muda wote, hatalikitokea janga au ajali yeyote kwenye biashara, vyombo vya usafiri na hatakwenye nyumba yako hautahangaika sana.
"Lakini pia kuna changamoto moja taasisi hizi za bima nanyimmerundikana mjini, ofisi zenu zipo Dar es salaam huku mikoani haumpo, ilimuwafikie wananchi wengi zaidi basi mjitahidi kuwekeza nguvunyingi maeneo ya vijijini, mkifanya hivyo elimu ya bima itaenea nchinzima na itakuwa na msaada kwa watu wote," alisema Mongella.
Mongela alisema ni ukweliusiopingika juhudi za elimu kwa bima zinaonyesha matundayake katikati ya mijini ispokuwa vijijini ambapoalisisitiza wakuu wa taasisi hizo kubadili mwelekeo nakuifuata jamii inapoishi.
Alisema kama mkuu wa mkoa amekuwa akitembelea vijiji na kuonahalisi ya jamii kutokuwa na elimu ya bima na wanapoelezwa wanaonyesha kuwa nauhitaji, hivyo ni wakati muafaka taasisi hizo kutambua asilimia 80ya watanzania wapo vijijini na kusisitiza kuwa lengo la Serikali nikufikia asilimia 50 kila mtanzania kuwa na bima ifikapo 2028.
Kwa Upande wake Rais wa Taasisi za Bima Tanzania (TIRA), James Bosco alisemakuwa ameguswa na maneno ya Mongela na kuahidi kwamba kuanzia sasa ataelekezanguvu kubwa ikiwa lengo ni kuhakikisha wanaifikisha elimu ya bimakwa kila mtanzania.
"Kuwa na bima ni kitu muhimu kwenye maendeleo ya uchumi wataifa lakini tumegundua kuwa katika pato la taifa bima bado haina mchangomkubwa, sasa ni wajibu wetu tulio ndani ya bima kutoa elimu ili watu wengizaidi waweze kuelewa shughuli zetu.
"Pamoja na kuyatumia maonyesho haya pia tunaahidi tutayafikia maeneoyote nchini ikiwamo vijijini ambavyo kwa kiasifulani hatujawahi kuonekana, hapa Mwanza tunatambua kuwakuna wavuvi na wakulima wengi hivyo watu kama hao wasijihisi kama bima haiwahusubali wanatakiwa wakate bima ili yanapotokea majanga yasiyotarajiwa na kupotezamali zao wasije wakaanza upya," alisema Bosco.
Kwa upande wake Kamishina wa Bima Tanzania, Musa Juma alieleza kuwa hadisasa asilimia 34 tu ya Watanzania ndio wenye uelewa na bima hivyo wao kamataasisi za bima wanaendelea kutumia njia mbadala hasa mitandao ya kijamii naujumbe wa simu ili kuongeza uelewa zaidi kuhusu bima nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.