Zaidi ya million 17 alizotapeliwa Mwalimu mstaafu zarejeshwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) yamrejeshea.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga alisema walipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa mwalimu mstaafu Masolwa Lukanda (62) amedhulumiwa mafao yake na mtu aitwaye Bosco Marwa (32)ambapo jumla ya million 32 zilichukuliwa kwenye akaunti yake kwa njia isiyo halali .
Alisema uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo ilibaini kuwa mzee huyo alikuwa ni mtumishi wa shule ya msingi Bulolambeshi iliyopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo alistaafu kwa lazima Julai 19 mwaka juzi na kulipwa mafao yake na Mfuko wahifadhi ya jamii PSPF Febuary 22 mwaka jana ,Mwl huyo alikuwa na mikopo halali kwenye taasisi za fedha na mikopo hiyo ilikatwa kwenye malipo yake ya kustaafu na kubaki na 40,603,821,92.
Aidha alisema mbali na mikopo ya taasisi za fedha aliingia mkataba wa mkopo baina yake na Mmiliki wa Zabo Microcredit Ltd Bosco Marwa na alikopeshwa 14,559,625 ambapo mkatapa huo wa Agosti 27 mwaka juzi haukuonyesha riba bali una masharti kuwa fedha za mikopo zitarejeshwa baada ya mkopaji kupata malipo ya kustaafu.
“Machi 12 mwaka jana mwl huyo alipokea hundi ya mafao yake ya kustaafu ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu wilayani humo alipotoka nje ya ofisi alimkuta Bosco Marwa anamsubiri na akamtaka waende moja kwa moja benki akamlipe fedha zake ambapo siku hiyo kulikuwa na tatizo la kiufunza hawakuwaza kutoa fedha hiyo ambapo kesho yake waliongozana hadi tawi la NMB Kenyatta jijini Mwanza ambapo Bosko alichukua Tsh 32,000,000 kurejesha deni la Tsh.14,5559,625 hivyo kupokea malipo yasiyo halali ya Tsh 17,440,375.”alisema Stenga.
Aliongeza kuwa baada ya uchunguzi wa kina kufanyika na kubaini ukweli wamalalamiko hayo mtuhumiwa alikiri kuchukua fedha hizo na kuagizwa azirejeshe mara moja tayari fedha hizo zimerejeshwa na kukabishiwa mwl huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amefurahiya na kuipongeza TAKIKURU kwa kazi wanayofanya katika Mkoa huo.
"Kwanza niwapongeze sana TAKUKURU kwa kazi kubwa na nzuri wanayoendelea kufanya kwenye Mkoa wetu,mmeona kwenye matukio mengi tu wamesaidia sana kupata mali za umma ambazo wakati mwingine zimechukuliwa kinyemela,mnakumbuka tukiwa katika zoezi la vyama vikuu vya ushirika mpala leo hapa,mnakumbika madeni ya wakulima kwenye sekta ya pamba TAKUKURU imefanya kazi kubwa sana Mkoani,"alisema Mongella.
"Leo tumeona tena fedha takribani milioni kumi na saba laki nne elfu arobaini mia tatu sabini na tano(17,440,375) Sh. za Kitanzania ambazo Mzee Masolwa Ngeleja Lukanda alitapeliwa au aliibiwa na Bwana Bosco Michael Marwa ambaye ana Kampuni ya Zabo Microcredit LTD. Huu ulikuwa ni wizi tu wa mchana," alisisitiza.
"Mimi nitoe rai hapa kuna dalili hata kwenye mifumo yetu wenyewe kina mazingira ya ovyo kwa sababu huyu mzee katika mazingira ya kawaida alitakiwa kuambiwa na mwajiri wake pale Halmashauri au mfuko wa PSPFkwamba fedha yako imetoka maana wale ndiyo walitakiwa kumlipa lakini inaonekana huyu bwana alikuwa na mlolongo wa kujua kule na alikuwa ameishapanga kumchukulia fedha huyu mzee sasa TAKUKURU wakapa taarifa kwa mtoa taarifa,msiri na tunamshukuru sana,"alisema Mongella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.