Serikali imeonya na kusema, walimu 381 na mafundi sanifu wa maabara 137 ambao mara baada ya maombi yao kupitishwa na kupangiwa kazi wanapaswa kuripoti katika vituo hivyo vya kazi walivyo pangiwa na watakaochukua fedha na kisha kutoweka kwenye vituo vya kazi watachukuliwa hatua kali za kishesheria ikiwapo kufikishwa mahakamani.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa E. Iyombe na kusambazwa kwenye vyombo vya habari na tovuti hii kufanikiwa kupata nakala yake imesema, wale wote waliopangiwa vituo hivyo vya kazi watatakiwa kuripoti katika vituo vyao kati ya tarehe 17 na 21 Julai, 2017.
“Mwajiriwa atakaye chukua posho ya kujikimu na badaye kutoripoti na kuanza kazi katika kituo chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria” imenukuliwa taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wale wote waliochaguliwa na kujiunga na utumishi wa umma watatakiwa kuripoti katika vituo vyao kazi wakiwa na vyeti halisi vya kuhitimu kidato cha nne na cha sita, cheti cha kuhitimu taaluma husika sambamba na cheti cha kuzaliwa.
Aidha taarifa hiyo imefafanua kwamba, hakuta kuwa na uhamisho ndani ya mkoa au wilaya bila idhini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), huku ikiwataka wakurugenzi wa Halmashauri kufanya taratibu zote za ajira na kuwasilisha taarifa ifikapo tarehe 25 Julai, 2017.
Ajira hizo zimetolewa kwa walimu wa Sayansi, Hisabati pamoja na Mafundi Sanifu kwa shule za Sekondari kwa awamu ya pili ikiwa ni adhma ya Serikali kuhakikisha inamaliza matatizo ya mahitaji ya walimu nchini.
Soma majina yote kupitia www.mwanza.go.tz
Majina.ORODHA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA (LABORATORY TECHNICIANS) WA SHULE ZA SEKONDARI WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI-2017-2.pdf,ORODHA YA WALIMU WENYE STASHAHADA AU SHAHADA YA SAYANSI NA HISABATI WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI AWAMU YA PILI-2017-2.pdf
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.