Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo TANESCO (TANESCO SACCOS LTD),Tawi la Mkoa wa Mwanza kimetoa msaada wa mashuka 140 kwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure Mkoa wa Mwanza.
Akikabidhi mashuka hayo Meneja wa TANESCO SACCOS LTD Taifa Andre Hilary amesema iko haja ya wadau wengine kuthamini watu wenye mahitaji maalumu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanesco kiliandikishwa mwaka 1843 na kupata namba ya usajili mwaka 1968 ambapo Uanachama ndani ya TANESCO SACCOS uko wazi kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme – TANESCO, Wafanyakazi wa TANESCO SACCOS, Wastaafu wa TANESCO, Wafanyakazi wa muda Maalum wa TANESCO, Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni au Taasisi zilizo katika sekta ya Nishati.
“Chama hiki kilianzishwa kikiwa na lengo la kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kuwapa fursa ya kukopa kwa riba nafuu kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi,”alisema Hilary.
TANESCO SACCOS kupitia mpango Mkakati wa miaka mitano 2014-2018 unatekeleza msingi namba 7 wa Ushirika wa kuijali jamii (Concern for the Community). Katika Mpango huo Chama kinatoa msaada katika sekta ya Afya kwa kutoa Mashuka katika Hospitali za Rufaa za Mkoa Nchi nzima.
Zoezi hili ni zoezi endelevu lilionza mwaka 2014 kwa taasisi ya magonjwa ya kansa ya Ocean Road na kuendelea na Hospitali zote nchini.
Mikoa iliyopatiwa msaada kwa mwaka huu ni pamoja na Mwananyamala RRH Dar es Salaam, Songea RRH Ruvuma,Amana RRH,Temeke RRH in Dar es Salaam,Dodoma RRH, Ligula RRH Mtwara, Mbeya Zonal RH, Mount Meru RRH Arusha, Morogoro RRH,hizi Hospitali zote zilipata mashuka 150 kila moja.
Hospitali ya Kitete RRH Tabora na Geita RRH ambao walipata mashuka 130 kila Hospitali wakati Hospitali ya Sekou Toure RRH imepata mashuka 140 na kukamilisha jumla ya mashuka 1750 yaliyotolewa hadi sasa.
Aidha, Dira ya TANESCO SACCOS ni kuwa SACCOS inayoongoza Nchini Tanzania inayokidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya wanachama wake kupitia huduma bora za kifedha ikiwa na Dhamira ya kuhamasisha na kuimarisha ukusanyaji wa akiba, hisa na amana kupitia utoaji wa elimu ya mikopo na huduma bora kwa wateja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.