• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TASAF Yatoa bilioni 3.2 Miradi ya Maendeleo Mwanza

Posted on: April 23rd, 2022

Katika  mwaka wa fedha wa 2021/2022 Mkoa wa Mwanza umepokea kiasi cha zaidi ya bilioni 3.2(3,213,430,392.23), kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 40 ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu,afya na ajira ya muda.

Huku katika kipindi cha miaka mitano Mkoa unatarajia kupokea kiasi cha zaidi ya bilioni 24.3(24,395,865,000) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kupunguza umaskini.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel,wakati akifungua kikao kazi cha kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa miradi ya kupunguza umaskini awamu ya nne(TPRP IV) katika mpango wa TASAF Mkoa wa Mwanza kilichofanyika mkoani hapa.

Mhe. Mhandisi Gabriel, amesema kati ya miradi hiyo 23 ni miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu,miradi ya afya 16 pamoja na mradi wa ajira za muda 1.

"Matarajio yangu ni kuwa mradi huu wa awamu ya nne utawezesha jamii kupata mafanikio ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya na elimu hasa katika kuwezesha watoto chini ya miaka mitano kuhudhuria kliniki na wanafunzi kuhudhuria shuleni," amesema Mhe. Mhandisi Gabriel.

Pia amewasisitiza, viongozi na wataalamu wote kuzingatia sheria,kanuni, taratibu na miongozo wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na usimamizi thabiti ili thamani ya fedha itakayotumika iendane na ubora wa miradi hiyo.

"Wakati wote wa utekelezaji wa miradi hii ni vyema kuhakikisha ubora wa miradi na thamani ya fedha ya miradi ionekane,pia nichukue fursa hii kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia kwa azma iliopo ya kuinua kipato cha kaya zenye changamoto ya kiuchumi,"amesema Mhe. Mhandisi Gabriel.

Kwa upande wake Katibu Tawala Masidizi- mipango na uratibu Mkoa wa Mwanza Joachim Otaru,amesema zoezi la uibuaji wa miradi ya kupunguza umaskini awamu ya nne(TPRP IV), ambapo jumla ya miradi 104 imeibuliwa na kupitishwa na Wizara kwa ajili ya utekelezaji.

Ambapo amesema kati ya miradi hiyo 31 ni ya afya,49 elimu na 24 ni miradi ya kutoa ajira za muda(PWP),jumla miradi hiyo itagharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 7.8(7,845,316,205.24).

"Miradi iliopokea fedha hadi sasa,Mkoa umepokea jumla ya bilioni 3.2(3,213,430,392.23), kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 40 ya ujenzi wa miundombinu ya elimu 23,afya 16 na mradi wa ajira za muda 1,"amesema.

Pia amesema,mafanikio yaliyopatikana  katika utekelezaji wa TASAF awamu ya tatu ni pamoja na kuwa na ongezeko  la mahudhurio  ya wanafunzi shuleni na kwa watoto wenye umri wa kuhudhuria huduma ya kliniki  kwa asilimia 95.

Kwa kuzingatia ruzuku inavyotolewa kwa kutimiza masharti ya kuhudhuria shule na kliniki ambapo jumla ya watoto 39,567 wametimiza masharti ya elimu na afya.

Naye Mratibu wa TASAF Mkoa wa Mwanza Monica Mahundi, amesema Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa mitano inayotekeleza miradi ya kupunguza umaskini awamu ya nne.

"Mkoa wa Mwanza jumla tumepokea fedha zaidi ya bilioni 3.2 ya kutekeleza miradi 40 ikiwa na maana ya miradi mitano kwa kila Halmashauri zilizopo mkoani hapa,ambayo inaanza utekelezaji muda si mrefu kuanzia sasa," amesema  Mahundi.

Amesema,kwa ujumla Mkoa wamejipanga kutekeleza miradi hiyo ipasavyo na kwa ufanisi na kufuata maelekezo na taratibu zilizotolewa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.