*TASAF yawa mkombozi kwa wasichana Mabuki, yawajengea Shule ya bweni*
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza Serikali ya Wamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha za Miradi nchini ikiwemo Ujenzi wa shule Maalum ya Wasichana Mwanangwa katika Kata ya Mabuki wilayani Misungwi.
Waziri Simbachawene ametoa pongezi hizo leo Agosti 04, 2023 wakati akikagua Ujenzi wa Shule ya Bweni ya Wasichana Mwanangwa chini ya Mradi wa kupunguza Umasikini awamu ya Nne kwa zaidi ya Milioni 138.8 uliounganisha vijiji vitano vya Mwanangwa, Ndinga, Mwagagala, Mhungwe na Lubuga vyenye jumla ya wakazi 15,252.
Amesema, kutoa fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kusogeza Elimu karibu ni uzalendo na ameonesha kuwajali watoto wa kike ambao awali wamekua wakitembea umbali mrefu na wamekua wakikumbana na vishawishi mbalimbali vilivyopelekea wakati mwingine kupata vishawishi na kupata Ujauzito na kukatisha masomo.
Aidha, amewaagiza TASAF na Halmashauri ya Misungwi kushirikiana kujenga wigo kwenye shule hiyo pamoja na njia za kupita wanafunzi kutoka Jengo moja kwenda jingine ili maeneo ya shule hiyo yawe nadhifu na yenye kuwapa mazingira ya usiri wanafunzi hususani wawapo kwenye maeneo ya bwenini na vilevile amewataka kupanda miti ili kulinda mazingira.
Naye, Mhe. Alexander Mnyeti Mbunge wa Jimbo la Misungwi ameishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi kwa kuleta fedha kwenye miradi na akabainisha kuwa wilayani humo kuna Shule mbili mpya zinajengwa na kwamba kwenye upande wa Afya, Maji, Miundombinu ya barabara na sekta zingine miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa.
"Vijiji hivi kwa pamoja viliafikiana shule kujengwa katika Kijiji cha Mwanangwa na kuibua miradi 10 yenye Majengo 6 Katika Mwaka wa kwanza wa Utekelezaji 2022 ikiwa ni Ujenzi wa Bweni la Wasichana, Bwalo, Madarasa 4, Ofisi na Matundu 12 ya vyoo, Jengo la Utawala na Maabara ya Biolojia na Kemia pamoja na nyumba ya Walimu 1 (2kwa 1)". Gloria Bunane Mratibu wa TASAF Misungwi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.