Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) watoa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa kuhusiana sekta ya usafiri wa anga wanafunzi wa shule za sekondari ya Nsumba na Nganza Mkoani Mwanza .
Akizungumza katika warsha ya kutoa elimu, Bi Thamarat Abeid Mkufunzi Mkuu Huduma za Viwanja vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kinachomilikiwa na TCAA anasema wanatambua vijana wanaihitaji kujengewa uelewa kuhusu sekta hiyo na fursa za ajira zilizoko kwenye sekta, hivyo anawataka wanafunzi hao kuzingatia masomo ya sayansi ili kufikia azma hiyo.
Ameongeza kuwa TCAA itaendelea kutoa elimu hiyo katika mikoa ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar ili kuwapa mwangaza utakaosaidia kunufaika kujiandaa vyema, kujiunga na hatimaye kunufaika na fursa za ajira katika sekta ya usafiri wa anga.
Naye Mwongoza ndege kituo cha kuongozea ndege kilichopo uwanja wa ndege Mwanza Bw. Benjamin Massery alisema elimu hiyo itawasaidia wanafunzi kutambua wasome masomo gani na ufaulu upi unaohitajika ili kuingia katika taaluma za usafiri wa anga.
" Tuna upungufu wa wataalam katika sekta ikiwa ni pamoja na marubani hivyo lengo letu ni kupata watu wengi hivyo elimu hii itaamusha chachu na kuzalisha wengi hapo tunawajengea uwezo hasa katika eneo la kuongoza ndege , wakati mwingine unakuta wanafunzi anajiuliza afanye nini, tumewapa elimu tambuzi ili mtambue atakayehitaji kuwa muongoza ndege asome kitu gani." Alieleza Massery.
Jofrey Osiro mwanafunzi wa Nsumba na Veronica John kutoka Nganza walisema vijana wengi wanapotea kwa sababu hawajapata ushauri kuhusiana na Mamlaka hiyo hivyo baada ya kufundishwa wamejifunza vitu vingi ambayo vinaweza kuwasaidia katika maisha yao.
' Mama yangu aliniambia ni vigumu sana kuwa rubani lakini mimi sijakata tamaa nina imani nitakuwa rubani ama kufanya kazi katika viwanja vya ndege leo nimejifunza vitu vingi nitayatekeleza kwa kufanya vizuri katika mitihani yangu nipate ufahulu wa juu ili nipate ufadhili wa masomo , nimefurahi sana kujua Tanzania kuna chuo kinachonifanya kutimiza ndoto yangu mwanzo nilitambua hakuna chuo hicho nchini sasa nitaitumia vyema fursa hiyo". Anaeleza John.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.