Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa msaada wa kompyuta 12 katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza ili kuhakikisha jamii za pembezoni zinanufaika na maendeleo ya sekta ya teknolojia ya Habari na mawasiliano(TEHAMA).
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha TEHAMA (TELESENTA) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi James M. Kilaba amesema kuanzishwa kwa kituo hiki ni faraja kwa TCRA kwani wamekuwa wakianzisha vituo kama hiki maeneo mbalimbali nchini na vimeleta tija kwa wananchi kwani vimechangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“TEHAMA imeleta mafanikio makubwa kwani wateja na watoa huduma wameongezeka katika eneo la simu za viganjani,huduma za intaneti,vituo vya televisheni na redio na ongezeko la huduma za kifedha kupitia simu za mikononi,”alisema Mhandisi Kilaba.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella katika uzinduzi wa kituo hicho amesema kuwa dunia sasa inaelekea kwenye uchumi wa kidijitali ambapo TEHAMA ni nyenzo muhimu ya kufikia maendeleo ya kiuchumi hivyo ni vema Nchi kuwekeza katika TEHAMA hususani kuijengea uwezo jamii ili iweze kukabiliana na mabadiliko haya ya utandawazi.
Hata hivyo Mhe.Mongella ameipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya na kuwashukuru TCRA kwa kufanikisha kuanzishwa kwa kituo hicho,pia amewataka Halmashauri ya Buchosa kuvitumia na kuvitunza viruri ili vilete tija kwa jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa WIlaya ya Sengerma Mhe.Emmanuel Enock Kipole amesema heshima ambayo wamepewa na TCRA wataienzi kwa kutumia vizuri vifaa kituo hicho kwani kulingana na tekinolojia inavyokua vifaa hivyo vitapelekea kukua kwa uchumi wa Wilaya ya Sengerema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.