TEKNOLOJIA YA MRADI WA ZAIDI YA PAMBA USAMBAE NCHI NZIMA: WAZIRI BASHE
Mradi wa Zaidi ya Pamba (BEYOND COTTON) uliokuwa ukifadhiliwa na Serikali ya Brazil umefungwa rasmi leo mkoani Mwanza huku rai ikitolewa na mwakilishi wa Waziri wa Kilimo ambaye ni Mkurugenzi wa usalama wa chakula Gungu Mibavu kusambaza teknolojia iliyotumika kwa mikoa inayolima zao hilo.
Akizungumza na wanufaika wa mradi huo katika hafla ya ufungaji huo iliyofanyika shule ya Sekondari ya Janeth Magufuli kijiji cha Nguge wilayani Misungwi Mibavu amesema lengo la mradi huo uliotekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu ni kuleta tija kwa mkulima wa Pamba.
"Niwaombe taasisi zote za utafiti wa kilimo mlioshiriki mradi huu,muhakikishe utaalanu wote unawanufaisha wakulima wa Pamba kuanzia kuwa na mbegu bora,pembejeo na ulimaji wa kisasa,"amesisitiza kiongozi huyo mwandamizi kutoka wizara ya kilimo.
Amesema kumaliza kwa mradi huo kuwepo sasa na matokeo chanya kwa wilaya za Misungwi,Magu na Kwimba ambapo mradi huo uliotekelezwa na kuwa mfano kwa maeneo mengine nchini.
Balozi wa Brazili hapa nchini Mhe.Gustavo Martines amebainisha nchi yake ina miradi ya mazao mbalimbali ikiwemo sukari na kahawa hivyo wataendelea kushirikiana na Tanzania kadiri ya uhitaji utakavyoonekana.
"Mradi huu wa Zaidi ya Pamba umekwenda pamoja na utoaji wa elimu ya umwagiliaji maji na lishe hivyo nimefurahi kuona hapa kijiji cha Nguge namna mnavyotekeleza kwa vitendo,"Balozi Gustavo.
Tupo katika mpango mkakati kwa kushirikiana na wadau kuanzia mwaka 2022 hadi 27 wa wa kutekeleza malengo ya kilimo kuanzia kuvuna hadi masoko,mradi huu wa Zaidi ya Pamba umekuwa sehemu ya mpango huo,"Sarah Gibson,Mkurugenzi mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula.
Awali katika mazungumzo mafupi na Balozi huyo mapema leo asubuhi Ofisini kwake, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Amos Makalla amesema ana imani mwisho wa mradi huu ndiyo mipango ya miradi mingine zaidi ya kilimo hasa kutokana na Brazil kupiga hatua zaidi ya teknolojia katika sekta hiyo.
"Tunahitaji pia elimu zaidi ya kitaalamu ya kilimo cha Sukari tuna ardhi nzuri yenye rutuba,tunapungukiwa na utaalamu wa kuzalisha kwa tija",mkuu wa mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.