Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameongoza Baraza la wafanyabiashara wa wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.
Katika baraza hilo, Mhe. Mongella amewataka wafanyabiashara kutumia baraza hilo kuainisha fursa na nini kifanyike kuondoa changamoto zinazowakumba wafanyabiashara kwenye maeneo yao huku akiwataka kufuata sheria bila shuruti.
"Ukiwa hufuati sheria, kazi ya Serikali ni kukushugulikia, unavoona Serikali imenyanyuka ujue kuna sababu"alisema Mhe. Mongella na kuongeza
" Lazima tujifunze sana kwenye massege ya juzi (kikao kilichofanyika ikulu kati ya wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini na Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli)"
Mhe Mongella aliyataka majukwaa ya wafanya biashara yawe na msaada na majawabu kwa wafanyabiashara na sio ajenda za vikao tu.
Naye Mdau wa masoko ya samaki Bonaventure Masambu aliitaka ofisi ya Mkoa kutenga eneo la soko ambalo litakuwa na bidhaa za samaki tu na mazao yake kwaajili ya watalii watakao taka kujifunza na kuangalia samaki, kwa wateja watakao nunua kutoka sehemu mbalimbali.
Mtengenezaji wa Wine Nyanza kusekwa aliwataka wafanyabiashara wakubwa wawe na upendo na mashirikiano kwa wafanyabiashara wadogo kwa kuwapatia mawazo ya kujiendeleza nasio kuwatenga ili kufikia Tanzania ya Viwanda.
Kwa Upande wa Meneja wa Sido Mkoa wa Mwanza Bakari Songwe aliwataka wakazi wa Mwanza kutumia fursa za viwanda vidogo vidogo kwa kutengeneza sabuni, samani za maofisini na fursa zingine zinazopatikana mkoani humo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.