TULINDE NGUVU KAZI YA TAIFA KWA KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA MARALIA: RAS BALANDYA
Viongozi wa Sekta ya Afya, Marafiki wa Maendeleo kwenye masuala ya Afya pamoja na viongozi wa dini wamekumbushwa kuunganisha nguvu pamoja katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Maralia ili kulinda nguvu kazi ya Taifa.
Rai hiyo ameitoa leo Aprili 29, 2024 na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balabdya Elikana wakati wa uhamasishaji wa kampeni ya ugawaji wa vyandarua Milioni 1.4 kwa Halmashauri 6 bila malipo zikiwalenga kaya zote ambazo zinakabiliwa na changamoto ya ugonjwa huo.
Balandya amebainisha kuwa licha ya takwimu kuonesha maambukizi ya Maralia kushuka kutoka asilimia 8 mwaka 2017 hadi 8% mwaka 2022 Mkoani Mwanza lakini bado nguvu ya ziada inahitajika kuutokomeza kabisa.
"Kwenye vituo vya afya bado kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa Maralia wanaofika kupatiwa matibabu, unakuta baadhi ya watu wanatumia vyandarua kuvulia samaki au kufugia kuku hii maana yake bado Jamii inahitaji mkazo wa kuelimishwa," Mtendaji wa Mkoa.
Aidha ameipongeza Wizara ya afya, Ofisi ya Rais- TAMISEMI pamoja na Marafiki wa Maendeleo kwenye sekta ya afya kuja na mpango huo ambao una nia njema ya kujenga afya ya Watanzania.
"Hapa tukumbushane tena wahusika wote katika ugawaji huu wa vyandarua tusiende kwenye kaya na kuanza kutanguliza masharti kabla ya kugawa, hapo tutakuwa tunapindisha malengo yetu," amesisitiza Balandya.
Aidha, ameitaka Jamii kuhakikisha inaunga mkono jitihada hizo za Serikali katika kampeni kama hizo na kuwaepuka baadhi wenye kauli potofu kuwa vyandarua hivyo vinapunguza nguvu za kiume ukivitumia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa amebainisha kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha elimu inatokewa kwa ufasaha kuanzia kwenye kaya hasa usafi wa mazingira wanayoishi.
"Kampeni hii imelenga Halmashauri za Buchosa, Kwimba,Magu, Misungwi, Sengerema na Ukerewe ambazo zimeonesha bado zinakabiliwa na changamoto ya Maralia", Stella Kajange,Mratibu wa Maralia na udhibiti wa wadudu wadhurifu OR-TAMISEMI.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.