Chuo cha Ulinzi cha Taifa chafanya ziara ya kujifunza mkoani Mwanza lengo likiwa kujionea hali halisi ya kiuchumi,kisiasa, kilimo, viwanda Mikoani.
Akizungumza Wakati wa utambulisho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John V.K Mongela amesema Mkoa wa Mwanza ni Miongoni mwa Miji Mikubwa inayokua kiuchumi kwa kasi Ukanda huu wa Afrika Mashariki wenye wakazi zaidi ya Milioni Tatu.
Mkoa wa Mwanza ni mlango wa Biashara kwa Majiji makubwa yalipo Afrika Mashariki kama vile Kisumu,Kampala, Kigali. Aidha Mhe Mongela amesema Mkoa wa Mwanza unafursa nyingi za uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo Biashara, Uvuvi na Ufugaji.
Akizungumza na waandishi wa Habari Msimamizi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa Luteni Jenerali Peter Paul Massao amesema chuo chao kimefanya ziara hii kwa lengo la kujifunza kwa vitendo na kujionea Uhalisia wa masuala ya Kiuchumi,Kisiasa, Viwanda na Kilimo baada ya kujifunza Chuoni.
" Tumekuja kujifunza ili kujionea hali halisi ilioyoko mikoani na kwenye wilaya zetu kisha tutaandika Taarifa ya tulichokiona pamoja na mapendekezo na kuyafikisha kwa viongozi kwa ajili ya ushauri" alisema Luteni Jenerali Peter Paul Massao
Ugeni huo utatembelea Kiwanda cha Nyama cha Chobbo, Mitambo ya uzalishaji Umeme Nyakato
Luteni Jenerali Paul Massao akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Zawadi yenye nembo ya Chuo cha Ulinzi cha Taifa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akimkabidhi Lt. jenerali Paul Massao zawadi yenye mchoro wa "Bismark Rock" mchoro unaoitambulisha Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.