TUMEPOKEA ZAIDI YA TRILIONI 4 KWA MIRADI YA KIMKAKATI MWANZA: RC MAKALLA
*Aishukuru Serikali ya Rais Samia ya kuzidi kujenga kiuchumi Mwanza*
*Asema miradi yote ikikamilika Mwanza itang'ara kiuchumi eneo la maziwa makuu*
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi leo Machi 22, 2024 ameipokea kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali na kuishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuleta mkoani humo zaidi ya Trilioni 4 kwa ajili ya miradi ya kimkakati.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Makilagi amesema Rais Samia ameonesha dhamira ya kweli ya kuupaisha kiuchumi mkoa huo kutokana na wingi wa miradi hiyo mikubwa.
"Mhe. Makamu mwenyekiti wa Kamati, Mkoa wa Mwanza kwa miaka mitatu mfululizo tumekuwa na Hati Safi hii maana yake tumetanguliza nidhamu ya matumizi yote sahihi ya fedha za Serikali na hata miradi hii mikubwa tunaisimamia vizuri na itamalizika kwa wakati," Mkuu wa wilaya.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe, Mhe. Japhet Hasunga amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kuletewa miradi Mikubwa na pia usimamizi mzuri wa miradi hiyo
"Mkuu wa Mkoa ni mfuatiliaji mzuri wa miradi sisi tumefika hapa kujiridhisha na matumizi sahihi ya fedha za Serikali sitarajii kukutana na changamoto zozote kutokana na usimamizi mzuri wa uongozi wa Mkoa", Mhe.Hasunga
Kamati hiyo ikiwa mkoani Mwanza itatembelea miradi saba inayotekelezwa na fedha za Serikali ukiwemo ujenzi wa Meli mpya ya Mv Mwanza na ukarabati wa Mv Victoria na Umoja, Ujenzi wa vivuko vya Serikali vinavyojengwa na kampuni ya Songoro Marine,na ujenzi wa Hoteli ya kitalii ya NSSF.
Miradi mingine ni huduma ya usambazaji maji Butimba, Jengo la mama na Mtoto Sekou Toure na Miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.