TUMIENI PROGRAMU YA GPE AWAMU YA TATU KUBORESHA SEKTA YA ELIMU: RAS BALANDYA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka wadau wa elimu kutumia programu ya kuboresha kada ya Ualimu (GPE) kuboresha mazingira ya ufundishaji ambayo ni pamoja na walimu kupata nyumba bora na vitendea kazi vya kufundishia.
Amezungumza hayo leo Machi 6, 2024 kwenye kikao kazi cha kutambulisha programu ya GPE awamu ya tatu kilichohusisha Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu, Maafisa Mipango na wadau wa Elimu Mkoani Mwanza.
RAS Balandya amewaomba wadau wote kutumia muda vyema kuhakikisha wanaifahamu programu hiyo vizuri na kwenda kuitekeleza kwa ubora ili kusaidia kutimiza malengo yanayokusudiwa na program hiyo.
“Tutumie muda vizuri kujifunza kwa ukamilifu kuhakikisha program tunaifahamu vizuri na kwenda kuitekeleza kwa ukamilifu na kuwafikishia wote watakaohusika katika utekelezaji ili malengo yaliokusudiwa yatimie” RAS Balandya
Naye Afisa Mawasiliano Serikalini kutoka TAMISEMI, Fredrick Kibano amebainisha kwamba program hiyo inayolenga kuborehsa kada ya ualimu itaanza utekelezaji wake mara tu baada ya kuzinduliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan huku akibainisha kuwa Tanzania ilijiunga kwenye mradi huu mwaka 2013.
“Mradi huu umejenga shule za msingi mpya zaidi ya 14 ambazo zimepunguza uhaba na kutoa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, ujenzi wa mambweni kwenye baadhi ya mikoa, pamoja na nyumba za walimu ili kupunguza uhaba” Kibano.
Vilevile, wadau mbalimbali wameupongeza mfumo wa programu hii kwa kuweza kuleta mabadiliko kwa kuboresha Sekta ya Elimu hususani kwa kuwakumbuka waalimu kwa kuwajengea nyumba za kuishi ambayo ilikuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya maeneo nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.