Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amepokea vyumba 2 vya madarasa Shule ya Msingi Bukandwe na matundu 12 ya vyoo na chumba maalumu kwa ajili ya kuhifadhia taulo za kike kwa wanafunzi wa kike, vilivyojengwa na Kampuni ya Mbogo Mining & General Supply Ltd kkwa ajili ya wanafunzi wa Shule hiyo.
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mhe. Mongella amesema Kampuni hiyo imefanya mambo makubwa ya maendeleo kwa ajili ya Wilaya hii.
"Tunahitaji wakina Mbogo wengi ili kuleta maendeleo ya shule zetu na Mkoa kwa ujumla,"alisema Mongella.
Awali akiongea wakati wa kukabidhi majengo hayo Meneja wa Usalama na Afya mahala pa kazi wa Kampuni hiyo Leone Eusebi Salekwa amesema Kampuni hiyo imetoa ajira kwa watanzania 63 na wamewapa kipaumbele wakazi wa Ihayabuyaga.
"Ujenzi wa chumba cha darasa Shule ya Msingi Bukandwe umegharimu Shilingi Milioni 45, wakati ujenzi wa matundu ya 12 vyoo na chumba maalumu cha kuhifadhia taulo za kike pamoja na taulo 100 umegharimu milioni 10.75," alisema Salekwa.
Aidha Salekwa ameongeza kuwa pamoja na makabidhiano hayo wamejenga pia chumba kimoja cha darasa katika shule ya msingi Bukandwe kilichogharimu Shilingi milioni 45, ujenzi wa matundu 12 ya vyoo na chumba maalum cha kuhifadhia taulo za kike pamoja na taulo 100 za kike ambazo zilikabidhiwa leo.
Tumejenga pia chumba cha darasa shule ya msingi Ilendeja chenye thamani ya sh.milioni 45,ukarabati wa choo cha walimu shule ya msingi Ilendeja kwa sh.milioni 4 , pia wametoa sare na vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 1,150 pia ukarabati wa shule ya msingi Ilendeja umegharimu Shilingi milioni 2,885.
Akiishukuru Kampuni hiyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Bukandwe Samiu Rugakingira amesema anaishukuru Kampuni ya Mbogo na anaomba Kampuni hiyo iendelee kuwa mlezi wa shule za msingi wa Bukandwe na Ilendeja.
Naye mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Bukandwe Jenifa Abuto aliyenufaika na ufadhili huo amesema Kampuni kama Mbogo ziendelee kuongezeka zaidi ili shule nyingi zaidi ziendelee kunufaika.
Akitoa salamu za Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Dkt. Philemon Sengati amesema Magu wanafanya mambo makubwa hawajawahi kumuangusha Mkuu wa Mkoa wa Mhe. John Mongella kwani hata uandikishwaji wa daftari la wapiga kura tumezidi asilimia tisini.
"Kata ya Bukandwe Mhe. Mkuu wa Mkoa ni asilimia 20 tu kwenye umeme na maji, tunakuomba wataalamu wako waje watusaidie wananchi wa Bukandwe baba tushike mkono Bukandwe,"alisema Michael Minzi ambaye ni diwani wa kata ya Bukandwe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.