TUNAISHUKURU SERIKALI YA RAIS SAMIA KWA KULETA MIRADI YA KIMKAKATI MWANZA: RC MAKALLA
*Miradi ikikamilika Mwanza itapaa kiuchumi*
*Kamati ya Bunge yaishauri serikali kujenga vituo vya afya Misungwi na Sengerema*
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amima Makilagi amesema Serikali imeleta Trilioni 3.3 kujenga miradi ya kimkakati kuanzia Daraja la JP Magufuli, Meli ya MV MWANZA, Uwanja wa ndege pamoja na Reli ya kisasa (SGR) ambayo yote kwa pamoja ni nguzo muhimu ya kiuchumi itakayo kuwa na tija kwa wananchi Taifa.
Mhe. Makilagi amesema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Machi 16, 2024 wakati akitoa salamu za Mkoa kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambapo ametumia wasaa huo kuishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuleta Miradi ya kimkakati ambayo amebainisha kuwa itapokamilika itaupaisha kiuchumi mkoa huo.
"Mwenyekiti wa kamati, Mhe. Moshi Kakoso kwa niaba ya wananchi wa Mkoa huu tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi na bunge kuiidhinisha ,tunakuahidi tutaisimamia vizuri na kukamilika kwa wakati," Mhe.Makilagi
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda vijijini Mhe. Moshi Kakoso amesema wataishauri Serikali kuhakikisha wananchi waliopitiwa na mradi wa Daraja la JP Magufuli wananufaika nalo kwa kujengewa vituo vya afya na Mkandarasi wa mradi huo.
"Wananchi wa wilaya za Misungwi na Sengerema tunakwenda kuishauri Serikali kabla ya mradi huu wa Daraja kukamilika wapatiwe vituo vya afya,naomba pia Ofisi ya mkuu wa mkoa hili mlisimamie na muhakikishe limefanyika," amesema Mwenyekiti wa kamati.
Aidha, ameutaka pia uongozi wa Mkoa huo kuhakikisha miradi yote haihujumiwi na wananchi na badala yake ikamilike kwa wakati na iwe endelevu kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.