Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa imefanikiwa kupata hati safi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizoidhinishwa na Serikali ambapo ilifanikiwa kupata hati hiyo (isiyo na mashaka) katika mapendekezo 35 yaliyotolewa ukilinganisha na mapendekezo 54 yaliyotolewa mwaka wa fedha 2017/2018.
Akiwasilisha utekelezaji wa hoja zilizotolewa na Ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na hesabu za Halmashauri za mwaka 2018/2019 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Crispin Luanda amesema kuanzia 2015 hadi 2019 mapendekezo yaliyotolewa ni 209,mapendekezo yaliyotekelezwa 128 ,yanayoendelea kutekelezwa 51,yalipitwa na wakati 37 huku yasiyotekelezwa ni 11.
"Tumepokea maelekezo tutaendelea kuchapa kazi pia baada ya miezi michache tunatarajia kuamia katika jengo letu la ofisi jipya tunalojenga"alisema Luanda.
Naye Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Dkt. Charles Tizeba amemuhoji Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hoja zinazojitokeza za kuleta madhara katika jamii ambapo Mkaguzi wa hesabu za Serikali amesema kuwa mara nyingi hutolewa maelekezo kwa menejimenti kufuata taratibu zinazostahili ili kunapokuwa na madhara yasiweze kujitokeza wakati mwingine.
Akitolea ufafanuzi kuhusu pale inapojitokeza kuwepo kwa muingiliano wa maslahi binafsi kuingilia katika kazi,Mkurugenzi wa Halmashauri Crispin Luanda amesema zipo sheria zinazowaongoza ili wasiweze kuingilia katika kazi mfano TBA hawawezi kujenga majengo halafu wajikague wenyewe ni kinyume na utaratibu.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Emmanuel Tutuba amewapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kupata hati safi na kuwaasa waendelee kujipanga ili miaka yote wahakikishe wanapata hati safi.
"Katika Halmashauri changa zinazofanya vizuri katika miradi ya maendeleo Buchosa mmo mnafanya kazi nzuri ili Jambo lisiishie hapa bali liwe endelevu huu ni wakati wakuchapa kazi "anaeleza Tutuba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.