TWCC KANDA YA ZIWA WAMSHUKURU RC MTANDA KWA USHIRIKIANO
Uongozi wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Kanda ya Ziwa leo Januari 09, 2025 wamemtembelea Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda na kumshukuru kwa ushirikiano anaowapatia, kadhalika kuwawezesha kuelekea Mkoani Dar es Salaam kushiriki uchaguzi.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Ofisini hapo, Mkurugenzi wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Kanda ya Ziwa Bibi Happiness Mabula amesema anamshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa moyo wake wa ukarimu na kumuomba kuendelea kuwa mlezi wa chemba hiyo.
“Tunakushukuru na tumefanikiwa kushiriki maeonesho ya jua kali Sudan Kusini na tumewakilisha vyema Mkoa wa Mwanza licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa”.
Aidha amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia kupata usafiri ambao Mhe. Rais Dkt. Samia amekuwa akiwasaidia Wanawake wajasiriamali magari ya mizigo na magari ya abiria ili nao kama Kanda ya Ziwa bado hawajafikiwa na msaada huo hivyo wamewasilisha ombi hilo ili Mkuu wa Mkoa aweze kuwasaidia.
Akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashukuru na kuwapongeza kwa kuwa katika masuala ya biashara changamoto lazima ziwepo lakini hawajaweza kukata tamaa bali wamepata uzoefu.
Aidha kuhusu usafiri wa Mama Smaia amewahidi kufuatilia na atawaandikia barua rasmi ya umuhimu wa kupata usafiri huo kutokana na ukubwa wa Kanda, na amesema kwa maonesho yajayo atakaa na Maafisa Biashara ili waone namna watakavyowasaidia kwenda na kurudi salama.
“Ofisi yangu hapa kipo kitengo cha biashara na wao wataniunganisha mimi na ninyi na hakuna kitakachokwama na mimi nitaendelea kuwa mlezi wa chemba yenu”.
Sisi hatutafunga milango na hatutachoka kwamba wamekuja juzi tu mbona leo tena wamekuja? aah kwa sababu maisha hayasimami yanaendelea hivyo tutaendelea kuwapa ushirikiano Ameongeza Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.