WAZIRI wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amepokea injini mbili za ujenzi wa meli mpya ya ‘’Mv Mwanza hapa kazi tuu’’ na kuwataka wakandarasi waliopewa zabuni ya ujenzi wa meli hiyo kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha meli hiyo kwa wakati.
Alisema ni wakati wa wananchi kufaidi matunda na mambo mazuri yaliofanyika na serikali ,alitoa msisitizo kwa wananchi wote watakao husika katika utekelezaji wa mradi huo na watakaotumia miundombinu baada ya kukamilika kuhakikisha wanautunza ilivizazi vijavyo viweze kuitumia kwa kuwa inatokana na kodi wanazolipa
Akitoa taarifa ya ujenzi wa meli wa meli hiyo mpya mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za meli nchini ( MSCL) Erick Khamis anaeleza hatua zilizofikiwa za ujenzi wa meli mpya.”Mv Mwanza hapa kazi tuu”alisema hadi mradi umefikia asilimia 65 kwa usanifu meli na ujenzi huku uungaji wa chuma ikiwa ni asilimia 15 hivyo atua ya upokeaji wa injini ni atua muhimu katika utekelezaji wa mradi huo huku ukiashiria maendeleo makubwa.
Wah. John Mongella na Adam malima ni baadhi ya wakuu wa mikoa ambayo meli hiyo itafanya safari zake walisema miundombinu ya kimikakati itachangia kuleta kasi ya maendeleo ya nchi hivyo wananchi wa maeneo hayo wataitumia fursa hiyo kubwa itakayoleta tija kwenye shughuli za kimaendeleo .
Meli hiyo ya Mv Mwanza hapa kazi tuu kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 65 na imegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 89.7 ambapo inatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2021 na itafanya safari zake katika mikoa ya Mwanza,Kagera,Mara,na nchi za jirani ikiwemo Kenya na Uganda.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.