Wananchi wa Usagara na maeneo jirani wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanatarajia kupata neema ya usafiri wa moja kwa moja utakaowafikisha katika hospitali ya mkoa Sekou Toure na katikati ya jiji.
Hayo yalisemwa jana na Ofisa Leseni na Mkaguzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Mwanza ,Daniel Chilongani kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ,dini na wanasiasa kilichofanyika mkoani hapa alisema wapo katika hatua za awali za kuanzisha safari (roote) ya daladala ambazo zitakuwa za Usagara – Mzunguko zitakazokuwa zinapita katikati ya jiji na kuishia hospitali ya mkoa.
Chilongani alisema, wameamua kuja na mpango wa kuanzisha safari ( roote) hiyo ili kuwasaidia na kutatua changamoto ya usafiri kwa wananchi wa Usagara, kwani wakitaka kupata huduma katika hospitali ya Mkoa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya nauli na wanapata usumbufu wa kutumia gari zaidi ya moja kufika eneo husika.
Alisema, Sumatra katika kuhakikisha inaondoa hadha ya usafiri kwa wananchi wanategemea kuanzisha safari (roote) nyingine ambayo itatoka Kigongo Ferry kupitia katikati ya jiji hadi hospitali ya mkoa ambapo magari yatakuwa ni Kigongo Ferry – Mzunguko ambayo yatahusisha magari makubwa ( mabasi makubwa) yenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 25.
Pia alisema safari (roote) hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa daladala katikati ya mji pamoja na kuwapa fursa wananchi ya kupata usafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, ili waweze kuendelea katika shughuli za kimaendeleo na kupata huduma muhimu zinazopatikana makao makuu ya mkoa.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva Kanda ya ziwa, Hassan Dede alisema sumatra wanapoanzisha safari (roote) mpya washirikiane kwa pamoja katika kuhakikisha wanaelimisha madereva na kubandika stika zinazoonyesha mwanzo hadi mwisho wa safari.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.