Ujenzi rasmi wa meli kubwa kabisa katika ziwa Victoria waanza rasmi Baada ya kukamilika kwa uwekaji wa mkuku ( Keel Laying ) wa meli mpya ya "Mv.Mwanza hapa kazi tu "inayojengwa katika chelezo.
Akizungumza katika hafla hiyo leo Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za meli ( MSCL) Eric Hamissi anaeleza kuwa hiyo ndio hatua ya kuanza kwa ujenzi na uunganishaji wa msingi wa meli ili kupata msingi wote wa meli ,ambapo kwenye msingi huo utakuwa na kwenye vipande na una kina cha mita 3.75 ambacho ufikiwa wakati meli imebeba mzigo wote.
" Kukamilika kwa msingi huu wa meli kutawezesha ujenzi wa meli kwenda kwa kasi kuliko kasi ya awali ,kutokana nausanifu bora wa meli hii kampuni yetu inampango wa kuweka kumbukumbu za mradi mzima wa ujenzi wake katika maktaba zake kwa ajili ya vizazi vijavyo " anaeleza Hamissi
Ameongeza kuwa kampuni inayofanya kazi ya ujenzi wa meli hiyo inaitwa GAS Entec, na kampuni ya KANGNAM Corporation zote kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na SUMA JKT ya Tanzania kwa gharama ya Dola za kimarekani 39,000,000 sawa na shilling Billion 89.764 hadi sasa mradi umefikia kiasi cha asilimia 68 kwa ujumla wake na serikali imeshamlipa mkandarasi jumla ya shilingi za kitanzania billion 59.896 sawa na asilimia 68 ya gharama zote za mradi.
Naye Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Dk Leonard Chamiriho anasema hiyo ni hatua ya kwanza muhimu kwa maisha ya meli ,pia mpaka Sasa miradi mitatu imekamilika ambayo ni mradi wa Mv.Victoria ambayo kwa sasa inafanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Bukoba, ukarabati wa mkubwa wa Mv.Butiama na mradi wa chelezo.
" Mji wa Mwanza umenufaika na ujenzi wa meli hii kwani imetoa ajira kwa wingi lakini hapa tulipo Septemba 3 mwaka 2018 ilitiwa saini mikataba ya miradi minne ambapo miradi mitatu imekamilika " ameeleza Chamiriho.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewahakikishia usalama katika mkoa wake ili kazi zifanyike kwa utulivu na ueledi unaotakiwa ,pia ujenzi huo wa miundombinu ya kimkakati ya kiuchumi ni hatua moja wapo nyeti ya kufikia lengo.
" Juzi Rais Magufuli alipofika Mwanza kufanya Kampeni aliwaeleza wananchi nia yake ya dhati na ya serikali kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha kiuchumi kwenye Kanda za maziwa makuu na lengo hilo litatimia" anaeleza Mongella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.