Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amezindua kampeni ya Furaha Yangu na kuwataka wanaume wakapime ili kujua afya zao na kusisitiza itumike kubadili tabia kwenye jamii na kutoa matokeo chanya kwa kupunguza maambukizi mapya.
Pia alisema ushiriki duni wa wanaume kujitokeza kupima na kujua afya zao katika Mkoa huo ni changamoto ambayo hata katika ngazi ya Taifa ndivyo ilivyo lakini watambue serikali inawajali na haitawaacha nyuma kwenye kampeni hiyo.
Akizindua kampeni hiyo kwenye viwanja vya Furahisha katika Manispaa ya Ilemela Mongela alisema kampeni hiyo ni muhimu katika kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi mkoani Mwanza.
“Ili kufikia lengo hili muhimu ningependa kuona Mkoa wa Mwanza unashiriki kikamilifu kwenye kampeni hii na ubunifu wake utoe matokeo chanya ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa wetu ili kuongeza idadi ya wananchi waliopima VVU na kufahamua afya zao wapate matibabu ili kuokoa maisha yao,”alisema Mongella.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema wachache waliopima na kujua hali zao ni asilimia 74 tu wameanza kutumia dawa.Pia walioanza kutumia dawa na kufuata masharti ya dawa baada ya kubainika kuwa na VVU ni asilimia 72 na wamefanikiwa kufubaza virusi ingawa bado mwitikio wa wanawake ni mkubwa kuliko wa wanaume.
Alieleza kuwa kampeni ya Furaha Yangu inatoa jumbe wa matumaini kwa wanaoishi na VVU na UKIMWI kwani inasisitiza kupima na kuanza tiba mapema na matumizi sahihi ya dawa na kumfanya mwenye maambukizi iashi maisha marefu.
Mongela aliongeza kuwa ili wananchi wapate huduma hizo serikali imeamua kutoa bure huduma za vipimo, matibabu na dawa bila malipo na hivyo wajitokeze kupima na waanze matibabu mapema kwa waliombukizwa.
Awali kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Mwl. Khadija Nyembo alisema kuzinduliwa kwa kampeni hiyo kutawawezesha wananchi wa wilaya hiyo kupima VVU kwa wingi ikizingatiwa kasi yao ya upiamji ni ndogo.
Kwa upande wake Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele alisema upimaji huo uyafikie makundi maalumu ambayo yanaongoza kwa kuwa na maambukizi na kupatiwa dawa kinga kwa wasio na maambukizi ya VVU.
Alisema maambukizi ya VVU mwaka 2003 hadi 2011 kwa Mkoa wa Mwanza yalipungua kutoka asilimia hadi asilimia 4.2 lakini takwimu za mwaka jana yaliongezeka hadi kufikia asilimia 7.2 sawa na ongezeko la asilimia 75 kutokana na jamii kujisahau baada ya kiwango kushuka.
Alisema malengo ya serikali kiwilaya ni kufikia 90,90 90 kupitia mifumo chanya ya kubadilisha tabia ili ifikapo 2020 wawe wanafahamu afya zao kwa waathirika waanze dawa na waliokwisha anza kutumia dawa hizo za VVU vipungue na kutowaambukiza wengine ili 2030 kusiwe na maambukizi mapya.
Kwa mujibu wa Dkt. Hadi Machi 2017 wananchi wasiojua hali zao ni 93,916 lakini waliofikiwa ni 50,000 tu na kwamba dawa kinga ilianza kutolewa kwa makundi maalumu ambayo ndio yanayoongoza kwa VVU.
Kampeni ya Furaha Yangu yenye kali mbiu ya Pima, Jitambue, Ishi inatekelezwa na mradi wa USAID Tulonge Afya na FH 1360 inalenga kuhamasisha wanaume walio katika hatari ya kuambukizwa VVU na kuwashawishi wananchi walio kwenye hatari hiyo kupima na kujua hali zao ili kutokomeza mamambukizi ya VVU na UKIMWI.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.