Agizo la Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kutoa siku nne kutaka makontena yaliyo na vifaa vya ujenzi wa chelezo, ukarabati wa meli ya MV Viktoria na MV Bitiama yaliyokwama Bandari ya Dar es Salaam kufika jijini Mwanza limetekelezwa ambapo jana makontena 10 kati ya 56 yalipokelewa Mwanza.
Makontena hayo yalipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa, Katibu Mkuu wizara hiyo-Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamriho, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini ( MSCL), Erick Hamisi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mapokezi hayo, Mhe.Kwandikwa alisema anashukuru agizo la Mhe. Rais Dkt. Magufuli limetekelezwa ndani ya siku alizotoa ambapo makontena yote 56 yameondoka jijini Dar es Salaam kulekea Mwanza na kati ya hayo 10 yamewasili salama.
“Sisi kama wizara tulipokea maelekezo na tumeyatekeleza kwa wakati, kilichobaki ni kuona kazi ya ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli ya MV Viktoria na MV Butiama inaanza haraka na kukamilika kwa wakati tena kabl aya Machi , 2020, zaidi ya yote tunashukurua kwa ushirikiano uliafanyika tangu agizo litolewa hadi leo napokea mizigo hii,”alisema Kwandikwa.
Naye Meneja wa MSCL, Hamis alisema baada ya kupokea vifaa hivyo atasimamia kwa ukaribu kazi hiyo na itakwenda kwa haraka sana na kukamilika mapema huku akisisitiza hakutatokea kasoro katika ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli hizo.
Naye Mkuu wa Mkoa,Mhe.John Mongella alisema sasa hivi hakutakuwapo na majadiliano kwani tayari Mhe.Rais Magufuli ametoa maelekezo ujenzi huo kukamilika kwa wakati, hivyo hataweza kumvumilia mtu yeyote anayetaka kukwamisha shughuli hiyo.
Julai 16, Mhe.Rais Dkt. Magufuli aliagiza Wandarasi wa wanaotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo pamoja ukarabati wa meli za MV. Victoria, MV Serengeti na MV. Butiama kuhakikisha zinakamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia amemuagiza Msimamizi wa Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kusini, Moris Mchindiyuza kuangalia maslahi ya vibarua wanaopakia na kupakua mizigo kwenye bandari hiyo ikiwa ni pamoja na kusajili majina yao ili waunde chama chao kusimamia masilahi yao.
“Wahandisi na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano hakikisheni kazi hii inafanyika kwa ubora na umakini kwani haiwezekani Serikali ikatoa zaidi ya Sh. bilioni 152 kujenga meli na kukarabati nyingine halafu mradi unachelewe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.