Manspaa ya Ilemela imetakiwa kuanzisha miradi itakayowawezesha vijana kujiajili ili waweze kurejesha mikopo ipasavyo baada ya kundi hilo kutuhumiwa kutorejesha mkopo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi wakati wa kujadili utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa hesabu za Halmashauri kwa kipindi cha 2019/2020 kwa Manspaa hiyo.
Alisema baada ya hoja kueleza kutorejeshwa kwa mkopo iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake ,vijana na wenye ulemavu zaidi ya Milioni 156 huku Mkurugenzi wa manspaa hiyo John Wanga kueleza mikopo isiyorejeshwa ni vijana, kwani vijana hawarejeshi tofauti na akinamama ambao wanafanya vizuri kwenye urejeshaji.
Hata Hivyo Mhandisi Robert ameiagiza Manspaa hiyo kubuni namna ya utoaji mkopo ambapo wanaweza kuwaanzishia miradi ambayo itawajenga na kuweza kujiajili na kuajili vijana wengine .
" Vijana ni tofauti na akinamama wenyewe unaweza kuwapa fedha wakitoka nje wanagawana lakini mkiwawezesha wakafungua kiwanda mfano cha kufyatua matofali hiyo itawasaidia kujiendesha ,kuajili watu wengine na wakarejesha mkopo vyema na kuondokana na ilo tatizo" alieleza.
Aidha aliwasihi madiwani kufatilia miradi na kutokuweka mtu sehemu yenye mapato ,wadhibiti mapato kwa pamoja wawe kitu kimoja ,wanasheria kuwa wazalendo na kuwa na nidhamu kwenye fedha sambamba na wataalum kuwa na kasi ya kujibu hoja Kama mkaguzi alivyosema pamoja na kuongeza vyanzo vingine vya mapato ili waweze kujiimarisha zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi John Wanga amesema watahakikisha wanabuni miradi itakayowawezesha vijana kujiajili na kuondokana na mfumo uliokuwepo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.