*Viongozi wanaosimamia mamlaka za nidhamu watakiwa kutekeleza maagizo kutoka Tume ya Utumishi wa Umma*
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana amewataka viongozi wanaosimamia mamlaka za nidhamu kutekeleza kwa wakati maagizo kutoka Tume ya Utumishi wa Umma ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
Akifungua kikao kazi leo kwenye ukumbi wa Rock City Mall kilichowahusisha viongozi na watendajii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Elikana amesema wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakichangia uwepo wa migogoro kutokana na kukaidi maagizo ya Tume.
"Nimefurahi kuwaona viongozi mnaosimamia mamlaka za nidhamu kutoka Mikoa ya Mwanza,Geita,Mara na Simiyu,naamini kupitia kikao kazi hiki tutakumbushana haki na wajibu lengo ni watumishi wafanye kazi katika mazingira rafiki ili ufanisi wa kazi uongezeke,"Amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.
Balandya ameongeza kuwa Mhe.Dkt.Samia ndoto zake siku zote ni kuwaona watumishi wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili kuongeza ari ya uwajibikaji pia anataka kuwaona wakipewa elimu za mara kwa mara ambayo itachangia kuwajengea uwezo.
"Ndugu viongozi tutumie vizuri kikao kazi hiki kupata uelewa wa kutosha na muulize maswali pale mnapoona kuna utata wa tafsiri za miongozo,Tume hii imekuwa ikipokea mashauri mengi ambayo yamechangiwa na viongozi wa maeneo husika kushindwa kuzitafsiri vizuri Sheria zilizopo,"Mhe.Balozi Adadi Rajabu,kamishna wa Tume.
Kikao kazi hicho kimewahusisha Wakurugenzi wa Halmashauri,Wakuu wa Taasisi,wenyeviti wa Halmashauri na Mameya kutoka Mikoa ya Mwanza,Geita,Mara,na Simiyu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.