Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika kusimamia vizuri ushirika na kutatua changamoto zake.
Majaliwa aliyasema hayo kwenye madhimisho ya siku ya ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahisha Mkoani Mwanza huku kauli mbiu ikiwa "USHIRIKA KWA ULAJI NA UZALISHAJI ENDELEVU KWA BIDHAA NA HUDUMA”.
“Ushirka unatija kubwa kwa wakulima na nyie viongozi wenye dhamana ya kusimamia ushirika kwenye maeneo yenu Serikali inawategemea sana, na niwahakikishie tutakuwa pamoja katika kusimamia ushirika huu," alisema Majaliwa.
Majaliwa alizitaka mamlaka zote nchini zinazohusika na vyama vya ushirika kujiwekea malengo yanayotekelezeka ili kuvikuza pamoja na kushirikiana na viongozi wa vyama hivyo ili kudhibiti wizi, dhuluma na ulaji wa fedha za wanachama wa ushirika.
Aidha, aliwahakikishia wanaushirika kuwa, mazao yao yanathamani ndani na nje ya nchi nakuwataka kuendelea kuzalisha kwa wingi na ubora.
"Pamba, kahawa, korosho na tumbaku vyote hivi vinatakiwa na wanunuzi watakuja kutoka ndani na nje ya nchi wote wasimame kwenye bei nzuri ndio tutawauzia mazao," alisema Majaliwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.