• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Vituo vya Afya vyawezeshwa kutoa huduma bora Mwanza

Posted on: July 14th, 2018


Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameupongeza Mkoa wa Mwanza kwa kuongezeka kwa vituo vya afya vyenye nyota tatu kutoka kituo kimoja mwaka 2015 hadi vituo 116 mwaka huu na kupungua kwa vituo vyenye nyota ziro ambavyo vilikuwa 151 mwaka 2015 kufikia vituo saba mwaka huu.

Mwalimu amebainisha hayo alipokuwa akizindua Mpango mkubwa wa kuboresha Afya ya Uzazi kwa Wajawazito na Watoto (IMPACT) unaotekelezwa na Aga Khan Development Network kwa ufadhiri wa serikali ya Canada utakaogharimu shilingi Billioni 25 na kutekelezwa katika Halmashauri zote nane za wilaya 7 za mkoani Mwanza.

Mhe. Mwalimu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha vituo vyote vya afya Tanzania vinanyota tatu ili viweze kutoa huduma bora ikiwemo huduma ya uzazi ya mama na mtoto

“Wanawake wengi hawapendi kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma kwa sababu ya lugha chafu na huduma mbovu, unapoona namba ya wanawake inaongezeka maana yake wana imani kubwa na huduma inayotolewa katika vituo vya mkoa ambao wameongezeka kutoka asilimia 67 hadi asilimia 77,”alisema Mwalimu. 

Mhe.Ummy alifanya ziara  katika kituo cha afya kwa huduma mashuleni katika Kata ya Nyamagana na kuangalia changamoto za kituo hicho na kuwashauri halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia mapato yake ya ndani kuweka mkakati wa kuanza ujenzi wa kituo hicho kisha wizara itaweka nguvu baada ya kuona hatua za awali.

Awali akimkaribishaMhe. Ummy kwenye jimbo lake, Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula alisema wilaya ya Nyamagana ina ongezeko kubwa la wakazi wa Nyamagana ikiwa idadi ya watu wafikao 460,000 wanawake 217,600, wanawake waliofikia uwezo wa kuzaa ni 186,600 huku wilaya ya Nyamagana ikikadiriwa kuwa na wajawazito wapatao huduma 15,666.

Aidha, Mhe Mabula amepongeza serikali kwa kuwezesha kupata 96%-98% ya fedha ya madawa na vifaa Tiba kutokea 46% iliyokuwa ukipata huko nyuma. Mhe Mbunge amemuomba Waziri kupitia wizara yake kuangalia namna ya ongezeko la wakazi pamoja na Wagonjwa wa dhalura Nyamagana na pamoja na hospital ya Mkoa wa Mwanza inavyoweza kupelekea kuwa na changamoto ya ufanisi kazini.

Akitoa neno la shukurani Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe Bhiku Kotecha amepongeza ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM kwa vitendo katika Wizara ya Afya na kumshukuru  waziri kuzidi kuitendea haki wizara hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.