Viongozi Mkoa wa Mwanza wamewataka wanahabari Mkoani humo kuzingatia maadili ya uandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao.
Hayo yamebainishwa na Afisa Habari Mkuu wa Mkoa, Abel Ngapemba aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi kwenye mdahalo ulioendeshwa na Mwanza Press Club katika ukumbi wa Victoria Palace Mkoani hapo.
"Maadili ya uandishi wa habari,uhuru wa kujieleza na haki ya kupata taarifa vinajieleza katika katiba na Sheria ya Habari hivyo ni vema kuzitekeleza alisema Ngapemba."
Katika Mdahalo huo waandishi wa habari kutoka klabu za waandishi wa habari Mwanza, Geita, Mara na Simiyu na wadau mmbalimbali wa habari, kutoka TCRA walihudhuria akiwepo Mhandisi Francis Mihayo, huku Jeshi la polisi likiwakilishwa na Inspector Mwita Robert Mwita na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akiwakilishwa na Flora Magabe.
Pamoja na kujadili mambo mengi kuhusu sekta ya habari mkoani humo wajumbe waliokutana kwenye mdahalo huo wamekubaliana juu maazimio mbalimbali ikiwemo kuitisha mkutano wa wadau wa habari wa kanda ya ziwa kujadili changamoto zinazokabili tasnia ya habari na utatuzi wake, kuendelea kuboresha sheria zinazogusa tasnia ya habari nchini zikiwemo EPOCA ya mwaka 2010,Media Service Act ya mwaka 2016,Cybercrime na Statistics act na kuimarisha mahusiano kati ya waandishi wa habari na wadau wa habari hasa taasisi za serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.