Mkoa wa Mwanza umepokea wageni mbalimbali kwa ajili ya Mkutano wa fursa za uwekezaji wa Teknolojia ,Mitaji na Masoko ya madini uliojumuisha Wizara ya madini , Shirikisho la Vyama vya wachimbaji wadogo wa madini Tanzania ( FEMATA) ,wachimbaji na wadau wote wa madini nchini.
Mkutano huo unafanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall wenye lengo la kuwahamasisha wachimbaji kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya madini ili waweze kupata matokeo chanya yenye kuleta maendeleo .
Akizungumza katika warsha hiyo Raisi wa Shirikisho la Vyama vya wachimbaji wadogo wa madini Tanzania ( FEMATA) Mhe.John Bina aliwataka wafanya biashara kuwa wazalendo na kutochezea fursa walioipata na kuacha tabia ya kutorosha madini kwani kashifa hiyo itaichafua sekta nzima ya madini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko alisema mkutano huo unategemewa kuwa na mchango mkubwa katika sekta hiyo, hivyo wachimbaji wafuate na kuitakeleza kwa umakini taarifa zilizotolewa na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Kairuki,ili kuweza kuzitambua na kuzifuatilia fursa zilizopo nchini humo.
Aidha Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa Kairuki aliwataka wafanyabiashara kushiriki katika maonyesho ya kujitangaza pia wafahamu sheria na taratibu za uingizaji wa madini nchini China na wazifuate kikamilifu ili kuepukana na hasara na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Pia aliwataka kuwa makini na makampuni yanayojitangaza mitandaoni ili kuepukana na utapeli utakaoweza kujitokeza hivyo ni bora kuchukua taadhali kabla ya shali, pia juhudi za kuzungumza na makapuni yanayonunua madini nchini humo.
" Serikali tukiwa wajanja sekta ya madini na utalii vikiendana tutapata mapato mengi na kuweza kukuza uchumi wa nchi" alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wachimbaji madini Richard Selle alisema changamoto walionayo ni lugha hivyo amependekeza wachimbaji wote wanaokwenda Nchini China kutafuta masoko watumie mtandao wa 'We Chat' ili kurahisisha mawasiliano.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.