Wafanyabishara Mwanza watakiwa kuchangamkia fursa ya Maonesho kuboresha biashara zao
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza ametoa wito kwa wananchi wa Mwanza na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ili kujifunza.
Ametoa wito huo leo mchana tarehe 31, 08, 2023 kwenye viwanja vya Furahisha wakati alipotembelea Maonesho hayo na kutembelea mabanda ambapo amesema amebaini uwepo wa bidhaa za kisasa kutoka viwandani zilizoletwa na Mataifa ya Afrika Mashariki.
Amesema wananchi wakifika kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela watapata fursa ya kuona bidhaa hizo na kuweza kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa kufanya ubunifu.
Aidha, amewapongeza wadau mbalimbali waliofanikisha maonesho hayo huku akibainisha kuwa kwa Mwanza yamefana zaidi ya mwaka jana na kwamba kuna sababu ya kuendelea na mfumo wa wananchi kutolipia wakati wa kutembelea maonesho tofauti na ilivyokua ikifanyika katika miaka mingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.