Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amefungua kikao cha hafla ya kuwaapisha Wahandisi wa Kanda ya Ziwa na kuwataka kujitahidi kuishi kwa viapo vyao kwani kwa kukiuka kiapo ni kuvunja sheria.
"Unapoapa hadharani ni kuapa kwa Mungu wako,ishini viapo vyenu... niwaambie sehemu zenye Wahandisi wanawake kazi hufanyika kwa ubora zaidi hii inamaanisha wanaishi viapo vyao na kutunza uadilifu katika kazi wanazopewa,alisema Mhe.Mongella.
Aidha, Mongella ameongeza kuwa Wahandisi wanafanya kazi nzuri wajiamini mara nyingi hukesha katika kazi, hivyo wana uwezo mkubwa nawaasa wawe na moyo wa kuthubutu kwa kufanya hivyo watasonga mbele zaidi.
"Jitahidini kujenga misingi ya ujasiliamali katika fani mlizosomea,wengi mna uwezo wa kubuni na kufika mbali ila hamjapata mori ya uthubutu,alisema Mhe.Mongella.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB) Mhandisi Patrick Balozi amesema jukumu kubwa ya Bodi ni kusajili Wahandisi wa kada zote, kusimamia na kuratibu mienendo ya Wahandisi na shughuli zao zinazofanywa pamoja na Makampuni mbalimbali ya kihandisi.
"Bodi ya Usajili wa Wahandisi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Bunge namba 15 ya 1997 na kufanyiwa marekebisho chini ya sheria na 24 ya mwaka 2007, alisema Mhandisi Balozi.
Naye Hakimu Mkazi Mahakama ya Mkoa wa Mwanza Mhe.John Jagadi akitoa kiapo kwa Wahandisi hao amesisitiza kuwa Wahandisi watakaposhindwa kutimiza yale waliyoapa ndipo vyombo vya kisheria huchukua hatua staiki.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa huduma za Meli Tanzania Eric Hamissi amesema katika maeneo ambayo yanategemewa sana kwa maendeleo ni maeneo yanayosimamiwa na Wahandisi na kuwataka kuendelea kuwa waaminifu katika taaluma yao.
"Nashukuru mnapotutembelea katika miradi yetu mnakwenda kukutana na Wahandisi mbalimbali wakiwemo Wahandisi wa Cherezo ambao ni mradi mpya kwa hapa kwetu Tanzania naimani mtaongeza maarifa zaidi,alisema Eric.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.