Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Martin Nkwabi amewataka Wahandisi na Maafisa Ugavi wa Halmashauri kuwa waadilifu na kutekeleza Mradi wa BOOST kwa wakati na ufanisi.
Bwana Nkwabi ametoa kauli hiyo mapema leo tarehe 03.05.20223 Jijini Mwanza wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wahandisi na Maafisa Ugavi wa Halmashauri kuwa waadilifu na kutekeleza Mradi wa BOOST kwa wakati na ufanisi.
“kuna shida ya kimaadili ambayo wakati fulani inatufanya tuachane na utaalamu wa fani tulinayo, nisisitize umuhimu wa uadilifu na kuzuia mmomonyoko wa maadili katika utendaji kazi wetu, ninyi ni watumishi wa Umma msikwame kwenye tope la maadili” amesema Nkwabi.
Aidha, amewataka Maafisa hao kuzingatia vipaumbele na malengo ya Mradi huo wa Sekta ya Elimu ili kuondoa hoja za ukaguzi na kuukamilisha Mradi chini ya viwango stahiki kwani kwa kufanya hivyo kunaipotezea Serikali fedha nyingi ikiwa ni pamoja na kupata fedha za Wahisani.
Akiongea kabla ya mgeni rasmi, Joel Mhoja Mratibu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema Maafisa hao watapatiwa mafunzo ambayo yasaidia kuimarisha utendaji wao lakini pia kwenda kuwawezesha Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu ambao ni watekelezaji wa mradi huo moja kwa moja kwenye maeneo yao.
Akitoa neno la shukrani Mhandisi William Thomas Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi amesema watatekeleza mradi wa BOOST kwa weledi lakini ametoa rai ya kupatiwa gari ili kukabiliana na changamoto ya usafiri na kutoingiliwa na wanasiasa wanapotekeleza majuku yao kwenye ujenzi wa miradi.
Mafunzo hayo ya siku mbili kwa kanda ya Mwanza yanalengo la kuboresha ujenzi unaozingatia viwango kama ramani, ubora, rasilimali fedha na utunzaji wa mazingira ikihusisha washiriki kutoka Mikoa 12 ya Kagera, Kigoma, Tabora, Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Singida, Rukwa, Kigoma, Katavi na Geita
BOOST ni Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji wa kwa shule za Msingi na Awali Tanzania Bara unaochangia Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 202526 ambao ni sehemu pia ya Lipa kulingana na Matokeo (EP4R).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.