Mhasibu wa AMCOS ya MHEDI iliyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na wafanyabiashara 13 na madalili 3 washikiliwa na TAKUKURU Mwanza kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kinyume na sheria.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga alisema Mhasibu Paulo Nkuba alikuwa akisafirisha na kuuza dawa za kilimo zilizonunuliwa na serikali na kupelekewa Bodi ya pamba kwa lengo la kuwapatia wakulima wa pamba kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa madalali na wafanyabiashara wa maduka ya pembejeo za kilimo maeneo ya Lumumba Jijini hapa .
Alisema TAKUKURU ilifanya upekuzi kwenye madauka ya bembejeo za kilimo baada ya kupata taarifa kutoka bodi ya pamba na kubaini kuwa dawa hizo zenye thamani ya shillingi 12,609,000 zimeuzwa kwa wafanyabiashara hao kinyume na utaratibu .
"Baada ya kubaini changamoto hiyo tumefanya ufatiliaji na kutambua kwa nini pembejeo za kilimo haziwafikii wakulima kwa wakati kumbe kuna baadhi ya viongozi wa AMCOS wasio waadilifu wamekuwa wakiyauza madawa hayo kwa njia ya rushwa pia tumefatilia na madeni ya wakulima wa AMCOS na tumeweza kuokoa fedha nyingi ambazo zimehujumiwa na baadhi ya viongozi mbalimbali mkoani hapa"alisema Stenga.
Aliongeza kuwa baadhi ya viongozi hao wamekuwa wajizifanyia hujuma fedha za serikali kwa kuandaa vocha za usambazaji wa pembejeo hizo na kudai fedha nyingi serikali sambamba na kuwakata fedha wakulima na kutoziwasilisha serikalini pamoja kuwauzia wafanyabiashara badala ya wakulima.
Alisema watuhumiwa wote wamekwenda kinyume na kifungu 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11/2007 pamoja na kupatikana kwa mali njia isiyo halali kinyume na kifungu cha 311 cha sheria ya kanuni ya adhabu na marekebisho yake ya mwaka 2002 hivyo uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea kwa kuwabaini wote wanaohusika na ubadhirifu huu pindi uchunguzi utakapokamilika wahusika wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma ziazowakabili.
Aliongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu na hawatovumilia kuona upotevu wa fedha za serikali pia waliwataka wafanyabiashara wote kuacha tabia hiyo vinginevyo hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhusika na ubadirifu wa pembejeo za kilimo ,aidha wakulima watoe ushirikiano kwa TAKUKURU pindi wanapoona mambo hayaendi kwa utaratibu uliokusudiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa huo Mhe.John Mongella baada ya kupokea taarifa hiyo alisema tumeona pembejeo zilizokamatwa ambazo ni ruzuku ya serikali zinazotakiwa kwenda kwa wakulima moja kwa moja kwa sababu kuna kodi ya wananchi ilipelekwa humo ili kuinua sekta hiyo lakini baadhi ya watu wasio na uzalendo wameamua kuzifanyia biashara pembejeo hizo.
Hivyo aliwataka watanzania kuwa wazalendo na kutoa ushirikiano pindi wanapoona viashiria vya rushwa vinapotokea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.