Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amewataka wananchi wa Kitongoji cha Gana- Kamasi kufanya kazi kwa bidii na kuacha tabia ya kustarehe wakati wote ili waweze kumudu mahitaji ya familia na kujiletea Maendeleo.
Malima ametoa wito huo leo Novemba 05, 2022 alipofika Kisiwani humo kukagua Ujenzi wa Mradi wa Maji na Zahanati iliyo katika hatua ya Msingi inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambayo itawahudumia zaidi ya wananchi Elfu Sita wanaoishi katika kitongoji hicho kilicho kwenye Kijiji cha Kamasi.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Mkuu wa Mkoa ameiagiza kamati ya Ujenzi wa Zahanati kusimamia ujenzi huo kwa Uzalendo ili wananchi hao wapate huduma za Afya siku za usoni na sambamba na hilo amesema Mhe Rais Samia pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wamechangia jumla ya shilingi milioni 20 kwenye ujenzi huo.
"Naiagiza kamati ya ya Ujenzi wa Zahanati hii kusimamia ujenzi huu kwa uzalendo ili wananchi wetu wapate huduma za Afya na kuepuka usumbufu kwa kwenda Nansio kwa ajili ya kupata matibabu." Amesema Malima.
Kufuatia Agizo la Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa Oktoba 20 2022 la kumtaka ndani ya siku 15 Mkandarasi Intercounty Co LTD anayejenga Barabara za Kilomita 1 kwa kiwango cha Lami Nyepesi Wilayani Ukerewe ziwe zimekamilika Mhe. Malima amekabidhiwa rasmi Barabara hizo Mjini Nansio.
"Kama mnakumbuka Mkandarasi huyu alikua anasuasua kwenye Ujenzi hadi Mhe. Waziri Mkuu alimuita Dodoma Mkandarasi huyu na baada ya mazungumzo alipewa siku 15 kufikia leo awe amemaliza, nashukuru amekamilisha bado Mambo madogo tu kama taa ambazo ndani ya wiki moja zitawekwa.
Aidha, ametoa rai kwa wananchi kutunza Miundombinu ya Barabara hizo ili ziwasaidie kwa muda mrefu kusafirisha mazao na kuwawahisha kwenye majukumu lakini akawataka kufuata sheria za Barabarani ili kuepukana na ajali.
"Rai yangu kwa Wakandarasi wanaotekeleza Miradi, naomba sana wawe wazalendo wasipoteze muda na Rasilimali fedha za nchi kwani wakichelewesha miradi wanachelewesha pia Maendeleo ya wananchi." Mhe. Ally Mambile, Mwenyekiti wa CCM (W) Ukerewe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.