Walimu 68 kutoka Zanzibar wapo Mwanza kwa ziara ya Siku Tano.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya Elikana ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kuratibu safari ya Viongozi na Walimu waliofika Tanzania Bara kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kwenye mambo mbalimbali.
Ametoa pongezi hizo alasiri ya tarehe 09 Agosti, 2023 wakati akizungumza na ugeni wa timu hiyo wapatao 68 waliofika Mkoani Mwanza kutoka Zanzibar ambao pamoja na shughuli za kielimu wametembelea miradi ya maendeleo na vivutio vya utalii katika kuunga Mkono Filamu ya Royal Tour.
Amesema Taifa lolote linaendelea endapo kunakua na elimu bora kwa wananchi wake hivyo ndio maana kwa pamoja Serikali zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mapinduzi Zanzibar zinajikita katika kuboresha miundombinu na taaluma ili kuhakikisha wanafunzi wanapata
elimu bora.
Ndugu Elikana, amepongeza timu hiyo kwa kuamua kutembelea pia miradi ya maendeleo kama mradi wa Daraja la Kigongo-Busisi ambalo linatekelezwa kwa zaidi ya Bilioni 700 kwani wamejionea kwa macho namna gani mikao ya kanda ya ziwa itafunguliwa kupitia mradi huo ambao utakuza uchumi wa nchi na hifadhi ya Taifa ya Saanane.
"Natumia wasaa huu kumpongeze Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza vema nchi yetu kwani anaonesha kwa vitendo nia yake ya kulipeleka Taifa hili mbali zaidi kimaendeleo lakini pia Rais Dkt.Hussein Mwinyi kwa kazi nzuri nasi hatuna budi kuziunga miono juhudi za viongozi wetu hawa." Amesema Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Martin Nkwabi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.