Mwenge wa Uhuru leo Agosti 28, 2025 umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji katika kijiji cha Maligisu unaotekelezwa na Serikali Kuu chini ya usimamizi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa Tshs.915,644,987 ambao umefikia asilimia 90 ya ujenzi wake.
Akizungumza na wananchi katika kijiji hicho, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Bw. Ismail Ali Ussi amewapongeza Viongozi wa Wilaya hiyo kwa usimamizi wa mradi unaotekelezwa na Mkandarasi Ursino Limited ambaye mpaka sasa amelipwa Tshs. 529,307, 738.
Bwana Ussi amesema mradi huo ni chachu ya maendeleo kwani wananchi watatumia muda mwingi kwenye shughuli za uzalishaji tofauti na awali walipokua wakitumia muda mwingi kutafuta maji katika maeneo ya mbali ambako walihatarisha hata uhai wako kutokana na uwepo wa wanyama wakali.
Aidha, amewaagiza wananchi kulinda na kuithamini miundombinu hiyo kama serikali ilivyojitoa kuwaletea maji hayo basi wana wajibu wa kuwa walinzi kwa na kutoruhusu kuharibiwa kwa namna yoyote ili utumike kwa muda mrefu.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Arch. Ng’hwilabuzu Ludigija amesema wananchi wa Maligisu wamekombolewa kwani wameteseka na adha ya maji kwa muda mrefu kutokana na jografia ya ukame iliyopo na hata kuhatarisha maisha yao kwa kuliwa na wanyama wakali kama Fisi wanapotoka alfajiri kusaka maji.
Meneja RUWASA Wilaya ya Kwimba Mhandisi Godliver Gwambasa amesema wananchi 8488 watanufaika na mradi huo wa kisima kirefu cha mita 71 kwani una uwezo wa kuzalisha lita 7200 kwa saa na kwamba mradi huo umelenga kuongeza upatikanaji Maji Safi na salama kutoka 20% had8i 80%.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.