Wananchi Mkoa wa Mwanza wameandaa mbio ambazo zitafanyika kesho Oktoba 25, 2025 zikianzia uwanja wa Furahisha hadi hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure zilizolenga kutoa pole kwa wagonjwa mkoani humo na kujenga afya pamoja na kupongeza maboresho yaliyofanyika katika sekta ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2025 Meneja wa kituo cha michezo Bilo Ndg. Hamisi Bilali amwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuja kuziungamkono mbio hizo amabazo zitaambatana na zoezi la kupima afya pamoja na kufanya usafi katika hospitali hiyo.

Ndg. Athumani amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 200 na ameishukuru serikali ya Mkoa idara ya afya kwa kukubali na kuunga mkono tamasha lao ambalo limebeba kauli mbiu ya afya yangu mtaji wangu twende tukapige kura.
Ameongeza kuwa wamehamasika kuandaa tamasha hilo kutokana na mafanikio na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta ya afya Mkoani mwanza sambamba na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amewashukuru wadau wa michezo kwa kuleta wazo la mbio hizo ambapo amesema sekta ya afya ndani ya Mkoa huo inalipokea jambo hilo kama tunu ya kuchagiza afya bora kwa jamii.

Amesema tamasha la mbio hizo za pole zenye lengo la kujenga afya na kupongeza maboresho katika sekta afya mkoani Mwanza zinasawili kwani katika kipindi chamiaka minne tumeshuhudia maboresho ya zaidi ya asilimia mia moja kuanzia ajira mpya, miundombinu, madawa na vifaa tiba.

Akitolea mfano wa maboresho katika sekta ya afya mganga mkuu amesema mwaka 2021 mkoa ulikua na vituo vya kutolea huduma za afya 322 lakini hivi sasa serikali imejenga vituo hadi kufikia 573.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.