WANANCHI WA NGUDAMA - MISUNGWI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUJENGEWA BARABARA
Wananchi wa kata ya Bulemeji na Idetemia Wilayani Misungwi wameishukuru Serikali inayongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 8 kwa kiwango cha changarawe pamoja na daraja vinavyogharimu zaidi ya Milioni 427.
Shukrani hizo za wananchi zimetolewa leo ijumaa septemba 13, 2024 kwenye ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa wakati akikagua mradi wa daraja linalounganisha vijiji vya Ngudama na Kaluluma linalojengwa kwa zaidi ya milioni 122 katika kijiji cha Ngudama.
Akiongea kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Bulemeji Mhe. Rahma Emanuel amesema mradi huo umewapa heshima wananchi ambao awali walilazimika kulipa zaidi ya Shilingi elfu 7 kwa usafiri wa pikipiki kutokana na ubovu wa barabara lakini kwa sasa wanatumia Tshs. 2000 pekee.
Katika wakati mwingine Mhe. Mkuu wa Mkoa amekagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 6, Matundu 10 ya vyoo na Ofisi ya Walimu kwenye Shule mpya ya Sekondari Mwasonge inayojengwa kwa zaidi ya milioni 121 kutoka serikali kuu (Sequip) na akaagiza ukamilishaji unaozingatia ubora.
Aidha, katika kituo cha mabasi cha Misungwi Mhe. Mkuu wa Mkoa amekagua mradi wa ujenzi wa vyumba 20 vya maduka vilivyojengwa kwa zaidi ya milioni 79 kutoka fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo umebuniwa kwa ajili ya kusaidia kuongeza mapato ya Halmashauri kwa kupangisha na kwamba zaidi ya Milioni 8.5 zinatarajiwa kukusanywa kwa mwaka.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kuwataka wananchi kutunza amani na kujiandaa kushiriki kilele cha Mwenge wa Uhuru 2024 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mhe. Mtanda amekagua jengo la Mionzi kwenye kituo cha Afya Misasi lenye thamani ya Milioni 68 na amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo ambayo pamoja na vifaa tiba vinagharimu milioni 302.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.