Wananchi mkoani Mwanza waobwa kujitokeza kupima virusi vya Ukimwi ( VVU) hususani wanaume katika uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu ili kutambua hali za afya zao .
Wito huu ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa alisema, kampeni hiyo itazinduliwa julai 21 mwaka huu katika viwanja vya furahisha ikiwa na lengo kutoa taarifa, kuielimisha na kusaidia jamii ya mkoa huo kwa kupima VVU na kutoa matibabu ya kurefusha maisha iwapo watagundulika kuwa na maambukuzi .
. " Nawaomba wakazi wa Mwanza kuungana na mimi katika kampeni hii hasa wanaume wawe katika mstari wa mbele kupima na kujua afya zao watakao gundulika waanze kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo na kuwafanya wenye maambukuzi kuishi maisha mrefu wakiwa na afya ,kupunguza uwezekano wa kuwambukiza wengine kwa urahisi pamoja na kuishi wakiwa na furaha wawapo kazini, nyumbani na kwa jamii," alisema Mongella.
Alisema katika takwimu za mkoa huo kufikia lengo la tisini tatu (90,90,90) zinaonyesha kwa 90 ya kwanza ni asilimia 53 wanafahamu hali zao hivyo ni wazi idadi kubwa ya wananchi bado hawajui hali zao za maambukizi ,90 ya pili waliopimwa na kugundulika kuwa na virusi na kuanza kutumia dawa ni asilimia 74 , takwimu zikioyesha wanawake wapo wengi kuliko wanaume.
Pia alisema kwa 90 ya tatu takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 72 ndio walioanza kutumia dawa hizo kwa kufuata utaratibu ambao umewasaidia kufubaza virusi hivyo hizo zikiwa ni takwimu za kufikia march 2018 huku zikionyesha wanawake ni wengi kuliko wanaume, bado wanakazi kubwa ya kufikia malengo hayo huku matumaini yakiwa kufanikisha jambo hilo kupitia kampeni hiyo.
"Kampeni hii imefadhiliwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, TAMISEMI,USAID kupitia mradi wa miaka mitano wa FH1360- Tulonge Afya (Uhamasishaji),TACAIDS na ILO kipengele cha kufikia wanaume wenye umri zaidi ya miaka 45," alisema Mongella.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa alisema, mkoa huo kwa sasa kiwango cha maambukuzi VVU yamepanda kutoka asilimia 4 hadi 7.2, hivyo inaonyesha jinsi jamii ambavyo haijitokezi kupima na kutambua afya zao ,sasa wanakuja na mkakati wa kupunguza maambukizi mapya.
Dkt. Rutachumbizwa alisema, baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo zoezi hilo litafanyika kwa kina ndani ya miezi miwili katika halmashauri zote 8 za mkoa huo.
Alisema, wamefanya utafiti na kugundua kuwa maambukizi ya virusi hivyo kwa asilimia kubwa yapo maeneo yenye mikusanyiko ikiwemo sehemu za wavuvi, wafanyabiashara, makundi mabalimbali ya watu wanatumia madawa ya kulevya na wanaofanya biashara ya ngono .
Pia alisema serikali imetoa fedha nyingi katika sekta ya afya ikiwemo suala la VVU,hivyo Wananchi wajitokeze kwenye zoezi hilo ambalo ni bure kuanzia kupima na kupatiwa dawa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.