WANAWAKE MKOANI MWANZA WAFANYA MATENDO YA HURUMA KWA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUMU KATIKA SHULE YA MSINGI MITINDO - MISUNGWI
Katika kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani, wanawake Mkoani Mwanza leo Machi 06, 2024 wamefanya matendo ya huruma kwa kutoa bidhaa za zaidi ya Milioni tatu kwa watoto 275 wenye uhitaji maalum katika shule ya msingi Mitindo wilayani Misungwi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Bi. Hellen Boghohe ametumia wasaa huo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele watoto wenye mahitaji maalum nchini kupitia programu mbalimbali.
"Hongereni sana walimu kwa kuwa na mioyo ya upendo hata ukija hapa usiku utakuta watoto ni wasafi, hongereni sana kwa kujitoa kwenu. Amesema MNEC Boghohe wakati akiwapongeza walimu kwa malezi bora kwa watoto.
Janeth Shishila, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza amewashukuru wanawake kutoka TANAPA Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane, MWAUWASA, RUWASA, TANESCO, UWT - Mwanza, CHAVITA, AMANI GIRLS, Compassion Tanzania, AHUKI, BODI YA UTALII TANZANIA, MSCL, NGOs zote za Mkoa wa Mwanza na sekta binafsi kwa kujitoa kuwafariji watoto.
Bidhaa zilizotolewa kwa uratibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali ni pamoja Mahindi, Mchele, Mafuta ya kupikia, Mafuta ya kupata, Sabuni, Dawa za meno, maji ya kunywa, unga pamoja na nguo.
Maadhimisho hayo ambayo yanafanyika Machi 08 kila mwaka, kimkoa mwaka huu yatafanyika Ijumaa ya wiki hii wilayani Misungwi huku yakichagizwa na kauli mbiu isemayoa ' Wekeza kwa wanawake kurahisisha Maendeleo ya Jamii na ustawi wa Taifa" ambapo Mgeni Rasmi atakua Mhe. CPA. Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.