Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Mb)amefanya ziara ya kikazi Mkoani Mwanza lengo ikiwa ni kufuatilia maendeleo ya Sekta ya Viwanda,ambapo ametembelea kiwanda kidogo cha kutengeneza barakoa cha Felister na kushuhudia shughuli za uzalishaji zikiendelea kiwandani hapo.
Akiwa katika kiwanda kidogo cha Feliste Mhe. Bashungwa amesema anatembelea ili kutoa uhamasishaji kwa washonaji wote nchini hususani wa vyerehani kwa ngazi zote kuendelea kushona barakoa huku wakifuata maelekezo ya Mamlaka ya dawa na vifaa tiba(TMDA) pamoja na TBS ili kushona barakoa zenye viwango vinavyo kubalika nchini.
"Naelekeza TBS na TMDA kwenda kwenye vyombo vya habari,kwenda mikoani na kutoa elimu kwa washonaji wa ngazi zote kuendelea kushona barakoa kwa ajili ya kuwapatia watanzania maeneo yote hata vijijini ziweze kupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu," alisema Mhe.Bashungwa.
Aidha amesisitiza kuwa amefika kwa mzalishaji mdogo ili kuonyesha mfano kuwa si lazima kiwe kiwanda kikubwa ndiyo lizalishe barakoa kwani hata kata na kijiji mmoja mmoja anaweza kutengeneza kwani kuna wanakijji pale kijijini wanaozihitaji kwa bei nafuu na kwa urahisi..
Kwa upande wa Mkurugenzi wa kiwanda hicho bi Felista Matoke Nyangwe amesema tumeona fursa ya kuchangia katika jamii katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa corona (Covod -19) na tukaanza uzalishaji wa vifaa tiba tajwa tangu mwezi machi na tumekuwa tukipeleka TMDA ili wathibitishe ubora wake kwa kufuata maelekezo waliyotupatia.
"Kwa sasa tunaweza kutengeneza barakoa pcs 35,000 kwa siku na tunayo ziada ya pcs 70,000 ndani,tunaweza kutengeneza coverall suit pcs 500 kwa siku pia faceshields 70,000 kwa siku moja," alisema Nyangwe.
Alisisitiza kuwa kwa barakoa wanazotengeneza unaweza kufua na kuzinyooshe pia changamoto iliyokuwepo ilitatuliwa na mganga mkuu mara baada ya kuwatembelea aliwapa ushauri wa material za kutumia na mashine ambazo zitawasaidia kurahisisha utengenezaji wake.
Nao watengenezaji wa barakoa wa kampuni ya Ushinaji ya Diva Vitenge Khadija Liganga amesema wanatengeneza barakoa za aina zote hadi za watoto na wamepata mafunzo maalum kutoka TMDA na wanafuata ubora ulioelekezwa.
"Tunatengeneza size mbalimbali hadi za watoto na tunaamini pia Serikali yetu inaongozwa na chama cha mapinduzi hivyo tumefanya special kwa ajili ya chama cha mapinduzi kama mliiona hii ilisambaa sana kwa waheshimiwa ni sisi tulitengeneza,"alisema Liganga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.