Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mwanza wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa changamoto zote zinazolikabili eneo hilo ili kuwaletea Maendeleo Wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike katika kikao kazi na Watalaam hao kilichofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa na amebainisha kuwa bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo za dawa kuchina kutokana na uagizaji usiozingatia uhitaji sahihi na kutokuwepo na takwimu sahihi za wagonjwa wa VVU.
"Hivi karibuni nimetoka kufanya ziara ya ukaguzi wa Sekta ya Afya Wilaya zote za Mkoa huu bado sijaimaliza Ilemela na Nyamagana nimejionea wahusika wakijisahau na majukumu yao kuanzia Mganga Mkuu wa Wilaya na wengineo hivyo basi vikao kama hivi vitumike kubadilika" amesema Samike.
Vilevile, Ndugu Samike amewakumbusha Wataalam hao kujenga tabia ya kutoka maofosini na kutembelea maeneo yenye Miradi ya Afya ili kujua na kuzitatua changamoto mbalimbali na siyo kusubiri hadi kiongozi wa juu afike.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Thomas Rutachunzibwa amesema Sekta ya Afya kwa Mkoa wa Mwanza inazidi kuimarika kutokana na Serikali ya awamu ya Sita kutoa fedha nyingi za Miradi na Vifaa Tiba.
Kikao hicho cha kupanga bajeti kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi Mkoani Mwanza kimewashirikisha Waganga Wakuu wa Wilaya, Waratibu wa Afya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi zisizo za Kiserikali zinazopambana na ugonjwa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.