Katibu Tawa wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana amewakumbusha Wataalam wa Afya kuongeza juhudi katika kutokomeza ugonjwa wa Kifua kikuu na Ukoma nchini.
Akizungumza leo Jijini Mwanza na Wataalam wa Sekta ya Afya wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kitaifa wa mwaka wa kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma, Balandya amesema kwa mujibu wa ripiti ya mwaka 2022 ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 zenye kiwango kikubwa cha ugonjwa wa Kifua kikuu hivyo bado kuna ulazima wa kupambana na janga hilo.
"Nitumie Jukwaa hili kuwapongeza kwa jitihada za kupambana na ugonjwa huu na kupata mafanikio ya kupungua idadi ya maambukizi ya Kifua kikuu kutoka wagonjwa 306 kwa kila watu 100,000 mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa 208 kwa kila watu 100,000 mwaka 2021," amesema Mtendaji huyo Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Ndg. Balandya ameishauri Wizara ya Afya kuweka utaratibu wa kuzishirikisha Sekta nyingine ili kuongeza nguvu ya pamoja ya kutoa elimu kwa Umma ili malengo ya kuutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030 yatimie.
Kwa upande wake Meneja wa Mpango wa kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma, Dkt. Riziki Kisonga amebainisha lengo la mkutano huo ni kupitia na kutafakari ugonjwa huo na kuona namna pia ya kushikisha Sekta nyingine.
Mkutano huo wa Kitaifa wa mwaka wa kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa Kifua kikuu na Ukoma unafanyika Mwanza kwa muda wa siku tatu ukiwashirikisha Wataalamu wa Afya na wadau wa Maendeleo kutoka Sekta hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.