Watanzania watakiwa kuwa wazelendo na waaminifu pindi wanapopata ajira kwenye miradi mbalimbali inayotelelezwa nchini ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan na kuitelekeza kwa vitenda kauli yake ya kazi inaendelea.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa awamu ya tano ( SGR LOT 5) Mwanza - Isaka alisema changamoto kubwa wanayoipata ni baadhi ya watu wanaopata fursa ya kufanya kazi kutokuwa waaminifu .
" Inabidi kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake nchi inakwenda kasi kwa sasa uzalendo,uaminifu unahitajika sana na Rais wetu anasimamia miradi hii yote kwa ukaribu sana kwa sababu jambo ili lipo kwa maendeleo" alisema Mongella.
Naye Naibu Meneja Mradi huo Mhandisi Alex Bunzu alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa njia Kuu ya Reli yenye urefu wa kiliometa 249 na njia za michepuo zenye jumla ya urefu wa kiliometa 92 ,pia shughuli za awali za mradi huo zimeanza ambapo Mkandarasi aliwasili maeneo manne kwa ajili ya ujenzi wa kambi Kuu za mradi.
" Katika Mkoa wa Mwanza Mkandarasi amewasilisha maombi ya maeneo mawili kwa ajili ya ujenzi wa kambi hizi katika Kijiji cha Feli Wilaya ya Misungwi na Kijiji cha Nkalalo Wilaya ya Kwimba " alieleza Bunzu .
Kwa upange wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Feli Johari Hassan alisema ombi lao kubwa ni vijana wa maeneo hayo na jilani kupewa kipaumbele wakati ajira zitakapoanza kutolewa kwani vijana wengi kwa sasa wapo mtaani hivyo wapewe kipaumbele na kusiwepo na ubaguzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.