WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM WAPATA BWENI S/M BUSWELU, MAJI BWIRU SEKONDARI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kujenga bweni la watoto 90 kwenye Shule ya Msingi Buswelu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum shuleni hapo.
RC Mtanda amesema ni utashi na utu wa hali ya juu wametumia viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kuwajali na kuwambuka walemavu na kuona wawajengee mazingira salama ya kusoma na malazi
"Ninaendelea kuwapongeza kwa kutenga shilingi milioni 172.5 huku Milioni 100 zikitokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo na 72 zikitoka serikali kuuz Hongereni sana".
Aidha akikagua maendeleo ya miti 3476 iliyopandwa mwaka 2023 kwenye Shule ya Sekondari ya Ufundi Wavulana Bwiru wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru amewapongeza kwa utunzaji na uendelezaji mzuri wa miti hiyo ambayo ni muhimu kwa kuhifadhi mazingira.
Aidha, amewashukuru wahisani kutoka The Desk and Chair faundation kwa kutoa fedha zaidi ya Tshs. Milioni 35 kufadhili mradi wa maji kwenye shule hilo yenye watoto wenye mahitaji maalumu kabla ya Halmashauri hiyo kutoa Tshs. Milioni 15.
"Uwepo wa mradi huu wa maji haoa shuleni itasaidia watoto kusoma katika usalama wa kiafya". RC Mtanda.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake Wilayani humo kwa kukagua barabara ya Kiyungi yenye urefu wa Kilomita 0.49 kwa Tshs. Milioni 499 iliyotekelezwa na Nyanza Road Works inayoanzia Mwaloni- Kabuhoro Mkuu wa Mkoa ametembelea pia Shule Mpya ya Kisenga na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.