Watanzania wametakiwa kutumia wataalam wa kilimo wakiwemo watafiti Kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo na yenye tija kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akizungumza leo kwenye ufunguzi wa maonesho ya Nane nane kwenye uwanja ya Nyamhongolo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwasa, Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kilimo kubadilisha hali ya maisha ya wananchi.
"Hii ni fursa ya pekee kwa wadau, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kutumia vizuri jukwaa hili kwa kufanya mageuzi kwenye shughuli za kilimo na biashara kwa ujumla kwani hata Taasisi za kifedha sasa zinawakopesha wakulima tofauti na hapo awali,"Dkt.Nyamahanga
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo Ndg.Emily Kasagara amesema kuwa maonesho hayo ambayo yanawashirikisha washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera yanasaidia kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji Kwa wananchi wa mikoa hiyo.
"Tunajivunia namna wananchi wanavyopata hamasa na maonesho haya kwani yanazidi kuwa na faida kwao, Serikali imetenga fedha nyingi kuhakikisha kilimo kinakuwa mkombozi wa ajira hasa kwa vijana,"Kasagara
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masalla ametoa rai kwa wadau kuunganisha nguvu na kutatua changamoto zilizopo uwanjani hapo.
Mikoa ya Mwanza,Geita na Mara inaunda Kanda ya Ziwa Magharibi kwa kushirikiana kwenye maonesho hayo ya Nanenane kila mwaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.