WATUMISHI MWANZA RS WATINGA STESHENI YA SGR DAR
Watumishi kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza mapema leo asubuhi wameanza safari ya kuhitimisha ziara yao kwa kutembelea Stesheni ya SGR na baadaye kupanda kuelekea Jijini Dodoma.
Mara baada ya kuwasili Stesheni ya Dar ijulikanayo kwa jina la Magufuli leo Februari 23, 2025 msafara wa watumishi hao ulipokelewa na mwenyeji wao Bw.Hassan Mbonde kutoka kitengo cha Mawasiliano na kuanza kuwapa taarifa ya mradi kabla ya kuwatembeza kwa baadhi ya maeneo muhimu kwenye jengo la abiria.
"Huu mradi hadi Dodoma umegharimu zaidi ya Trilioni 7 na utakapo kamilika hadi Mwanza utagharimu zaidi ya Trilioni 20, fedha hizi ni mkopo kutoka kwenye taasisi za kibenki za kimataifa," amesema Mbonde.
Amesema, hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za kuanza kusafirisha shehena kubwa ya mizigo ambayo ndiyo itaingizia faida zaidi shirika la TRC.
Aron Kalondwa kutoka Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza amebainisha huo ni uwekezaji ambao kila mtanzania ana kila sababu ya kujivunia na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.
"Awali tuliona kama ndoto sisi kuja kuwa na mradi wa kisasa kama huu zaidi ya kuuona kwa Mataifa ya Ulaya na kwingineko, natoa pongezi kwa viongozi wetu wa Kitaifa kwa kuwapigania watanzania maendeleo,"Janeth Shishila, Afisa Maendeleo ya Jamiii.
Watumishi hao wakiwa safarini kuelekea Jijini Dodoma wameshuhudia mandhari ya nchi yakiwemo mabonde, mito na milima inayotiririsha maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.