WATUMISHI SEKTA YA MAJI WATAKIWA KUWA WAWAJIBIKAJI
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amewataka Watumishi, Viongozi wa sekta ya Maji kuhakikisha wanatelekeza majukumu yao ipaswavyo kutokana na unyeti wa sekta hiyo.
Katibu Tawala ametoa rai hiyo mapema leo Februari 24, 2025 alipokuwa akiwakaribisha Viongozi na Wataalamu wa Sekta ya maji kutoka Wizara ya Maji Tanzania Bara na Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, waliowasili Mkoani Mwanza kwa lengo la kujifunza masuala ya kisekta.
Bw. Balandaya amesema Maji ni sekta nyeti na hayana mbadala hivyo amesema endapo sekta hiyo itafanya vizuri basi Taswira ya viongozi Wakuu wa nchi kwa pande zote mbili Bara na Visiwani itakuwa imelindwa na kuaminiwa na wananchi.
“sekta ya maji ni muhimu sana kwa wananchi, ni vyema tukafanye kazi kwa bidii, uaminifu na weredi wa juu, tukailinde taswira ta Viongozi wetu kwa wananchi”.
Halikadhalika amepongeza utaratibu huo bora na mzuri wa kutembeleana na kufanya vikao vya kisekta hali inayopelekea uwajibikaji na uimarishaji wa huduma ya maji nchini.
Akizungumza mara baada ya kupokelewa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar Bi. Mwanaloma Abdallah amesema ziara hiyo imebeba matarajio makubwa, Hata hivyo ameeleza katika kikao hicho kutasaidia utekelezaji wa miradi ambayo inahusiana na taasisi hizo.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Maji Tanzania, Bw. Prosper Buchafwe amesema ziara hiyo inalenga pia kuonesha na kujifunza jinsi ya kuendeleza mashirikiano kati ya Wizara hizo na kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi hizo kwa Wananchi.
Wizara hizo zinazoshabihiana ziko Mkoani Mwanza kwa ziara na Vikao muhimu vya kisheria ambavyo hukutana mara mbili kwa mwaka vyenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kupeana uzoefu, Aidha vikao na ziara hizo zinaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.