WATUMISHI WA MWANZA RS WATEMBELEA BWAWA LA UMEME LA MWL. NYERERE
Watumishi kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wameanza ziara yao ya kwanza mkoani Pwani kutembelea Bwawa la Mwl. Nyerere lililopo eneo la Rufiji.
Watumishi hao wapatao 33 wakiwa njiani kuelekea Bwawani walipata fursa ya kuwaona baadhi ya wanyama wakiwemo Twiga, Tembo na Nyati kwenye eneo la hifadhi ya Taifa ya Nyerere National Park hali iliyochangia furaha ya kuona vivutio hivyo vya utalii.
Mara baada ya kuwasili eneo la mradi walipokelewa na mratibu wa mradi huo Mhandisi Fidelis Almasi na kutoa taarifa fupi ya mradi huo ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Nyerere miaka ya 70.
"Huu ni mradi mkubwa ambao umeigharimu Serikali Tshs Trilioni 6 na upo asilimia 96 unaotoa megawati 2115 na mashine zote 8 kati ya tisa zinafanya kazi,nadhani nyie ni mashahidi usumbufu wa umeme kukatika kama ilivyokuwa awali umepungua kwa asilimia kubwa",Mhandisi Almasi
Ameongeza kuwa mradi huo ni kitega uchumi cha uhakika kwa Taifa kwani umeme unaofuliwa hapo ni mwingi ambao nchi utaweza kuwauzia Mataifa ya jirani kama Kenya,Rwanda na Uganda.
Watumishi kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa walizidi kuhamasika na baadhi kupata na mshangao wa aina ya hali ya juu ya teknolojia iliyotumika kwenye mradi huo wakati walipotembezwa kuanzia kwenye chanzo cha maji yaliyochepushwa kutoka mto Rufiji na sehemu ya kufuliwa umeme huku asili ya mto huo ukibaki kama ulivyo bila kuharibiwa mazingira yake
"Nichukue fursa hii kuwapongeza kwanza kwa uzalendo wenu mlioutanguliza wa kufanya kazi kwenye mradi huu,ni dhahiri haya ni mazingira magumu kuwa mbali na familia zenu,hakuna eneo la shule jirani zaidi ya kuwepo kwenye mbuga ya Taifa,huu ni mfano wa kuigwa na sisi tutakuwa mabalozi wazuri wa kuyasema tuliyo yaona,"Janeth Sishila,Afisa Maendeleo ya Jamii
Kwa upande wake Mhasibu Mkuu kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa Ndg. CP Abdul Bandamo amebainisha Serikali ya awamu ya sita inazidi kuleta mageuzi chanya ya kiuchumi mfano mzuri ni mradi huu,Rais Samia amekuwa akihimiza matumizi ya nishati safi na sahihi huu mradi utakuwa na tija kwa watanzania.
Mradi huo wenye mandhari ya kuvutia kuna eneo lipo kwenye mikoa ya Morogoro na Lindi.
Watumishi hao watahitimisha ziara yao Jumapili hii kwa kutembelea mradi wa Treni ya kisasa SGR Jijini Dar na baadaye asubuhi kupanda Treni hiyo hadi Jijini Dodoma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.